Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Maximilian Maria Kolbe
(
8 Januari
1894
–
14 Agosti
1941
) alikuwa
padre
wa
Kanisa Katoliki
na
mtawa
wa shirika la
Ndugu Wadogo
Wakonventuali
kutoka nchi ya
Poland
.
Katika
historia ya Kanisa
anajulikana kwa jinsi
allivyomheshimu
Bikira Maria
kwa jina la
Imakulata
, yaani
Mkingiwa
dhambi ya asili
.
Baada ya kuanzisha chama cha
Mashujaa wa Imakulata
huko
Roma
(
Italia
) na
Mji wa Imakulata
huko Polandi, alikwenda
Japani
kama
mmisionari
.
Wakati wa
Vita Kuu ya Pili ya Dunia
alifungwa na wafuasi wa
Unazi
sehemu mbalimbali na hatimaye katika
kambi ya wafungwa wa siasa
kule
Auschwitz
. Huko alijitoa
kafara
ya
upendo
na
uaminifu
kwa
Mungu
na
binadamu
kwa kushika nafasi ya mfungwa mwenzake aliyechaguliwa kuachwa bila
chakula
hadi kufa pamoja na wengine 9. Aliwaandaa hao wote kukabili
kifo
kwa
tumaini
la
Kikristo
na bila ya
chuki
, na alipobaki peke yake aliuawa kwa
sindano
ya
sumu
[1]
.
Papa Paulo VI
alimtangaza
mwenye heri
tarehe
17 Oktoba
1971
, halafu
Papa Yohane Paulo II
alimtangaza
mtakatifu
mfiadini
tarehe
10 Oktoba
1982
.
Sikukuu
yake ni tarehe 14 Agosti kila mwaka
[2]
.
Wewe umenipenda milele, tangu u Mungu;
hivyo umenipenda na utanipenda milele!...
Upendo
wako kwangu ulikuwepo hata kabla sijakuwepo,
na ni kwa sababu ya kunipenda, Mungu mwema, kwamba
umeniita kutoka utovu wa vyote nianze kuwepo!
- B. HANLEY, O.F.M., Maximilian Kolbe, Upendo uliokithiri ? tafsiri ya Parokia la Mt. Maksimilian Kolbe, Mwenge, Dar-es-Salaam ? ed. Benedictine Publications Ndanda Peramiho ? Peramiho 1992
- Rees, Laurence.
Auschwitz: A New History
, Public Affairs, 2005.
ISBN 1-58648-357-9
|
Makala hii bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuiongezea habari
.
|