John Howard Northrop ( 5 Julai 1891 ? 27 Mei 1987 ) alikuwa mwanakemia kutoka nchi ya Marekani . Hasa alichunguza mbinu za uchachushaji pamoja na vimeng'enya . Mwaka wa 1946 , pamoja na James Sumner na Wendell Stanley alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Kemia .