Ijumaa
ni siku ya sita katika
juma
(wiki) ya siku saba yenye asili ya
kiyahudi
-
kikristo
. Iko kati ya siku za
Alhamisi
na
Jumamosi
. Katika hesabu ya kimataifa ya
ISO 8601
ni siku ya tano.
Nchi kadhaa za Waislamu wengi zimeanza kutumia Ijumaa kama siku ya mapumziko kwa wafanyakazi na sehemu ya
wikendi
.
Katika muundo wa juma wa kibiblia Ijumaa ni siku ya sita. Kanuni ya
ISO 8601
ilibadilisha hesabu ya juma kufuatana na kawaida ya mapumziko ya "
wikendi
" kwenye siku za
Jumamosi
/
Jumapili
. Katika muundo huu Jumatatu hutazamiwa kama siku ya kwanza katika juma ya kazi hivyo inahesabiwa kama siku namba "1" ya wiki katika kalenda hata kama jumuiya za kidini zinasisitiza hesabu ya ki
biblia
na kawaida katika tamaduni nyingi inaendelea hesabu ya kale.
Jina la siku kwa Kiswahili na kwa lugha mbalimbali
[
hariri
|
hariri chanzo
]
Katika lugha ya
Kiswahili
jina la siku halina namba ndani yake. Inaitwa kufuatana na lugha ya Kiarabu na utamaduni wa Kiislamu "ijumaa" kutoka neno la
Kiarabu
??????
al-juma'a yaani siku ya "jumuiya" ya Waislamu kukutana pamoja kwa sala kuu ya Ijumaa mchana. Pamoja na
Alhamisi
ni siku ya pekee ya juma yenye jina la Kiarabu.
Majina ya siku zingine yameanzishwa upya katika Kiswahili kuanzia Ijumaa kuzitaja kama Juma-mosi, Juma-pili n.k.
Lugha nyingi za nchi za Waislamu zafuata kawaida ileile zikitumia neno hili la Kiarabu kwa mfano kwa mfano
Kiindonesia
ni "Jumat" au
Kitartari
ambayo ni
lugha ya Kiturki
ni "Com?a" na kwa Kiuzbekistan ni Ж?ма (juma).
Katika lugha nyingi za Ulaya jina la siku hutunza kumbukumbu ya miungu iliyoabudiwa zamani za dini za Kiroma au Kigermanik kama vile
Kifaransa
"Vendredi" (siku ya Veneri /
Venus
) au
Kiingereza
"Friday" (siku ya
Freya
).
Katika mfundisho ya Mtume Muhammad mojawapo ni kuitukuza siku hiyo ya Ijumaa, kwani ni siku tukufu iliyochaguliwa na Mwenyezi Mungu na kupatiwa umma wa mwisho.
Mtume Muhammad alikhusisha baadhi ya vitendo katika siku ya Ijumaa:
Kusoma Surat Sijdah na Surat Insaan katika swala ya Al-Fajiri. Imepokewa na Abu Hureirah {Alikuwa Mtume akisoma katika swala ya Al-Fajri siku ya Ijumaa (Surat Sijdah) katika rakaa ya kwanza. Na katika rakaa ya pili (Surat Insaan)} Muslim.
Kusoma Surat Al-Kahfi. Amesema Mtume. {Mwenye kusoma Surat Al-Kahfi siku ya Ijumaa, Mwenyezi Mungu anampa mwangaza baina ya Ijumaa mpaka Ijumaa nyingine}. Al-Bayhaqi na Haakim.
Kuzidisha kwa wingi kumsalia Mtume Muhammad. Amesema Ibnu-Qayyim: “Mtume wa Mwenyezi Mungu ni Bwana wa viumbe vyote, na siku ya Ijumaa ni bwana wa siku zote. Kumswalia Mtume siku hii ina malipo mengi kushinda siku nyingine”.
Kuzidisha kumuomba Allah katika siku hii. Kwa sababu kuna wakati wa kukubaliwa dua ya Muislamu. Amesema Mtume: [Hakika katika Siku ya Ijumaa kuna wakati, haafikiwi Muislamu na wakati huo hali akiwa anamuomba Allah, ila Mwenyezi Mungu humkubalia Dua yake]
|
Makala hii kuhusu mambo ya
sayansi
bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu
Ijumaa
kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|