Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Biafra
ilikuwa jamhuri iliyojitenga na
Nigeria
kati ya
1967
hadi
1970
iliyotambuliwa na nchi chache tu na kurudishwa Nigeria baada ya vita kali. Eneo la Biafra ilikuwa katika kusini-mashariki ya Nigeria inayokaliwa na
Waigbo
hasa wakati ule lilitwa "Mkoa wa Mashariki" lililokuwa moja kati ya mikoa mitatu ya Nigeria baada ya uhuru.
Katika Januari
1966
ilitokea ghasia katika Nigeria. Sehemu za jeshi zilipindua serikali wakamwua waziri mkuu
Abubakar Tafawa Balewa
aliyekuwa wa asili ya kaskazini. Kiongozi wa serikali mpya alikuwa jenerali mkuu wa jeshi la Nigeria
Johnson Aguiyi-Ironsi
aliyekuwa Igbo ambaye mwenyewe hakushiriki katika uasi. Lakini katika miji ya kaskazini ya Nigeria raia Waigbo walitafutwa na kuuawa ovyo. Waigbo maelfu walikimbia katika miji ya kaskazini na kukimbilia kwao nyumbani walipoleta habari za mauaji.
Uasi wa pili ulifuata haraka tarehe
29 Julai
1966
na safari hii kikundi cha maafisa kutoka kaskazini walimwua Ironsi na kuchukua serikali mkononi mwao chini ya uongozi wa jenerali
Yakubu Gowon
. Mwaka uliofuata
1967
serikali mpya ilianza kubadilisha muundo wa utawala; mikoa mitatu ya Nigeria iligawiwa kuwa majimbo 12. Waigbo walisikitika ya kwamba mipaka ilichorwa kwa kusidi la kuacha maeneo ya Delta penye mafuta ya petroli nje ya majimbo penye Waigbo wengi. Ili ilitazamiwa kama jaribio la kuwatenga Waigbo na malighafi hizi.
Mwaka huohuo wa 1967 mauaji mapya ya Waigbo yalitokea katika kaskazini. Katika hali hii afisa kiongozi wa jeshi katika mkoa wa mashariki
kanali
Emeka Ojukwu
tar.
30 Mei
1967 alitangaza uhuru wa mkoa wa mashariki ulioitwa sasa "Jamhuri ya Biafra". Nchi chache tu zilitambua nchi mpya zilikuwa
Gabon
,
Haiti
,
Cote d'Ivoire
,
Tanzania
na
Zambia
.
Vita ya miaka mitatu ilianza 6 Julai 1967 jeshi ka serikali ya Nigeria iliposhambulia. Serikali ya Lagos ilipata msaada kutoka Urusi na Uingereza. Ufaransa, Ureno na Afrika Kusini zilisaidia upande wa Biafra lakini bila kutambulia nchi rasmi. Usaidizi hasa wa Urusi uliotoa
ndege za kijeshi
za aina Ilyushin IL-28 na mabomu ya Napalm uliwapa Wanigeria nguvu zaidi. Jeshi la anga la Biafra ilikuwa na ndege ndogo tu za kiraia zilizobadilishwa kubeba silaha.
Vita ilisababisha njaa kali na wakazi milioni 2 - 3 wa Biafra walikufa kutokana na njaa na magonjwa. Tarehe 13 Januari 1970 mabaki ya jeshi la Biafra yalijisalimisha mjini
Amichi
. Rais Ojukwu alikimbia kwenda Cote d'Ivoire.
Baada ya mwisho wa vita hofu ilikuwa kubwa ya kulipizwa kisasi lakini serikali ya Lagos ilijitahidi kujenga upatanisho na amani upya. Ojukwu alirudi Nigeria mwaka
1980
.