Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Belgrad
(
Kiserbia
:
Београд
-
beograd "mji mweupe"
) ni
mji mkuu
wa
Serbia
. Iko kando la
mto Danube
mahali ambako
mto Sava
unapoishia humo. Ni pia mji mkubwa wa nchi mwenye wakazi 1,710,000 (mwaka 2002).
Mji umejulikana tangu zamani za Dola la Roma kwa jina Singidun ulipokuwa mji wa
kikelti
. Waroma walijenga mji wa kiroma palepale kwa jina la Singidunum. Tangu kufika kwa Waslavoni mji ulipata jina "mji mweupe" au "boma nyeupe" kwa lugha mbalimbali.
Belgraf ilitawaliwa na nchi mbalimbali kama vile Bulgaria, Bizanti na Hungaria. Serbia ilianza kuenea hadi shemu hizi tangu karne ya 13. Mwaka
1403
ilitangazwa na
Stefan Lazarevi?
(1389-1427) kuwwa mji mkuu wa Serbia ambayo wakati ule ilisukumwa kaskazini kutokana na mashambulio ya
Waosmani
.
Tangu mwaka 1521 Belgrad ilivamiwa na Waturuki walioendelea kuitawala hadi karne ya 19 hata kama mju ulikuwa mahali pa mapigano mengi kati ya Uturuki na Austria ikatwaliwa na kupotelewa na Austria mara tatu katika karne zile.
1817
ilikuwa mji mkuu wa Utemi ya Serbia iliyofufuka tena. Imebaki hivyo hadi leo. Wakati ambako Serbia ilikuwa sehemu ya
Yugoslavia
ilikuwa pia mji mkuu wa Yugoslavia.
-
Beogradyanka - nyumba ya kisasa
-
Mt. Sava - kanisa orthodoksi kubwa duniani
-
Nyumba ya Benki Kuu ya Serbia
-
Bunge la Serbia
-
Mji wa Kale
-
Daraja la reli
|
Makala hii kuhusu maeneo ya
Ulaya
bado ni
mbegu
.
Je unajua kitu kuhusu
Belgrad
kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|