'
Andre-Marie Ampere
|
---|
|
Amezaliwa
| (
1775-01-20
)
20 Januari 1775
Lyon
,
Ufaransa
|
---|
Amefariki
| 10 Juni 1836 (umri 61)
Marseille
,
Ufaransa
|
---|
Kazi yake
| Mwanafizikia
|
---|
Andre-Marie Ampere
(
20 Januari
1775
?
10 Juni
1836
)
[1]
alikuwa
mtaalamu
wa
fizikia
na
hisabati
kutoka
Ufaransa
.
Ana umaarufu kama mtu aliyeweka misingi muhimu kwa
sayansi
ya
usumakuumeme
. Katika mfumo wa
vipimo sanifu vya kimataifa
kipimo
cha
mkondo wa umeme
kimepewa
jina
lake na kwa
Kiswahili
kinaandikwa
ampea
.
Alizaliwa nchini Ufaransa wakati wa
Zama za Mwangaza
.
Baba
yake aliyekuwa
mfanyabiashara
tajiri
hakumtuma
shule
bali alimpa nafasi ya kujisomea
nyumbani
.
Mwaka
1799
alipata
ajira
ya kwanza kama
mwalimu
wa hisabati na mwaka
1802
aliitwa kuwa mwalimu wa fizikia na
kemia
mjini
Bourg-en-Bresse
.
Baada ya
kifo
cha
mke
wake mwaka
1803
alihamia kufundisha kwenye
chuo
cha
Ecole Polytechnique
mjini
Paris
. Huko alipewa nafasi ya
profesa
mwaka
1809
ingawa hakuwahi kusoma shuleni wala chuoni wala kuwa na
digrii
yoyote.
Mwaka
1820
Ampere alijifunza kuhusu kazi ya
Mdenmark
Hans Christian Ørsted
aliyegundua ya kwamba
sindano
ya
dira
inaathiriwa na
mkondo wa umeme
unaopita karibu nayo. Hapo Ampere alianza
uchunguzi
kwa lengo la kuelewa uhusiano baina ya
usumaku
na
umeme
.
Alijumlisha matokeo yake mwaka
1827
katika
kitabu
Memoire sur la theorie mathematique des phenomenes electrodynamiques uniquement deduite de l’experience
(
Kumbukumbu
ya
nadharia
ya kihisabati kuhusu matukio ya dainamia umeme, iliyofikiwa hitimisho kwa njia ya maarifa na majaribio). Kitabu hiki kiliweka msingi kwa jina la sayansi mpya kuwa "dainamia umeme" (
electrodynamics
).
Mwaka
1827
Ampere aliheshimiwa kwa kuchaguliwa mwanachama mgeni wa
Royal Society
wa
Uingereza
na mwaka
1828
kama mwanachama wa
Akademia ya Sayansi ya Uswidi
.
[2]
Kwa heshima ya kazi yake kipimo cha
mkondo wa umeme
kiliitwa "ampea", pamoja na
coulomb
,
volti
,
ohm
na
watt
. Vipimo hivi viliitwa kwa heshima ya wataalamu waliofanya kazi pamoja na Ampere na hao walikuwa
Charles-Augustin de Coulomb
wa
Ufaransa
,
Alessandro Volta
wa
Italia
,
Georg Ohm
wa
Ujerumani
na
James Watt
wa
Uskoti
.
Jina la Ampere liko kati ya majina 72 yaliyoandikwa kwenye
Mnara wa Eiffel
mjini Paris.
Katika miaka yake kwenye vyuo mbalimbali alifundisha hisabati, fizikia,
falsafa
na
astronomia
.
Alikuwa
Mkristo
Mkatoliki
tena
Mfransisko
aliyechukua muda kujisomea katika
Biblia
hasa wakati wa matatizo maishani.
[3]
Kabla ya kufa mwaka 1836, Ampere aliagiza kauli ifuatayo iandikwe kwenye jiwe la
kaburi
lake: "Tandem Felix" (kwa
Kilatini
: "Hatimaye mwenye heri").
- Considerations sur la theorie mathematique du jeu
,
Perisse
, Lyon Paris 1802,
[1]
- Tafsiri ya Kiingereza ya baadhi ya mandishi yake:
- Magie, W.M. (1963).
A Source Book in Physics.
Harvard: Cambridge MA. pp. 446?460.
- Lisa M. Dolling, Arthur F. Gianelli, Glenn N. Statile, mhr. (2003).
The tests of time : readings in the developement of physical theory
. Princeton: Princeton University Press. ku. 157?162.
ISBN
978-0691090856
.
{{
cite book
}}
: CS1 maint: multiple names: editors list (
link
)
.
.
- Hofmann, James R. (1995).
Andre-Marie Ampere
. Oxford: Blackwell.
ISBN
063117849X
.
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
- Ampere and the history of electricity
- a French-language, edited by CNRS, site with Ampere's correspondence (full text and critical edition with links to manuscripts pictures, more than 1000 letters), an Ampere bibliography, experiments, and 3D simulations
- Ampere Museum
Archived
18 Aprili 2008 at the
Wayback Machine
. - a French-language site from the museum in Poleymieux-au-Mont-d'or, near
Lyon
,
France
- O'Connor, John J.
;
Robertson, Edmund F.
,
"Andre-Marie Ampere"
,
MacTutor History of Mathematics archive
,
University of St Andrews
.
- Catholic Encyclopedia on Andre Marie Ampere
- Andre-Marie Ampere: The Founder of Electromagnetism
- Background information and related experiments
Persondata
|
NAME
|
Ampere, Andre-Marie
|
ALTERNATIVE NAMES
|
Ampere, Andre-Marie (English)
|
SHORT DESCRIPTION
|
French physicist and mathematician
|
DATE OF BIRTH
|
22 January 1775
|
PLACE OF BIRTH
|
Polemieux
,
Lyon
,
France
|
DATE OF DEATH
|
10 June 1836
|
PLACE OF DEATH
|
Marseille
,
France
|