Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kamusi Elezo ya Kiswahili
|
Karibu kwenye Wikipedia ya Kiswahili!
Wikipedia
ni mradi wa kuandika
kamusi elezo
kamili na sahihi ya maandishi huru.
Kila mtu anaweza kuhariri makala yoyote, kutoa makosa ya lugha, kutohoa maneno na kuendeleza na kukuza makala, kwa kuandika kwa ufupi au kwa urefu. Tunakushauri ujiandikishe na
kufungua akaunti
. Angalia
Wikipedia:Mwongozo
ili ujifunze unavyoweza kuhariri au kusanifisha ukurasa. Usisite kushiriki; kwa sababu huu ni mradi wa ushirikiano, na hautaisha kamwe. Kamusi elezo itaimarika vizuri zaidi kila wakati. Angalia
ukurasa wa jumuia
,
ukurasa wa jamii
, na ule wa
makala za msingi za kamusi elezo
ili kung'amua unaweza kufanya kazi zipi ili kuboresha Wikipedia.
|
Je, wajua...
|
|
|
|
Makala ya wiki
|
Vimondo
(pia:
meteori
au
meteoridi
) ni
magimba madogo ya angani
yanayozunguka
jua
. Yanaweza kuangukia
duniani
yakionekana kama
moto
angani. Ukubwa wa kimondo ni kuanzia
punje
ya
mchanga
hadi kufikia
kipenyo
cha
mita
kadhaa. Hivyo kimondo ni kidogo kuliko
asteoridi
na kikubwa kushinda
vumbi la angani
.
Obiti
ya kimondo inaweza kuingiliana na obiti ya dunia au
sayari
nyingine. Kimondo kikilikaribia gimba la angani kubwa zaidi kinavutwa nalo.
Kikikaribia mno dunia yetu kinaingia katika
angahewa
na kuanguka chini kwa
kasi
kubwa sana. Njiani kinapashwa moto kutokana na
shindikizo
la
hewa
dhidi yake. Kiasi cha
joto
kinatosha kuchoma kabisa kimondo kidogo hewani. Hii inaonekana kwa macho matupu kama mstari wa moto angani. Kama kimondo ni kikubwa zaidi ni sehemu zake za nje tu zinazochomwa na
kiini
kinagonga
uso
wa dunia.
Kati ya vimondo kumi vikubwa kabisa duniani ambavyo mabaki yake yanaonekana, kimojawapo ni
Kimondo cha Mbozi
nchini
Tanzania
.
?Soma zaidi
|
|
|
Picha nzuri ya wiki
|
TANGAZO LA KIFO cha
Ingo Koll
au
Kipala
kilichotokea tarehe 10, Julai, 2023 nchini Ujerumani. Kipala alikuwa mchangiaji mashuhuri wa Wikipedia kuanzia Disemba 2005 hadi Juni 28, 2023. Siku kumi na mbili mbele tangu kuhariri Wikipedia yetu kwa mara ya mwisho, Mola Jalali Muumba wa mbingu na ardhi, alitwaa kiumbe chake. Kipala atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa wa kuhariri Wikipedia hii. Kwanza akiwa kama msimamizi (admin) baadaye mrasimu (bureaucrat) ambaye ametoa haki za usimamizi kwa wakabidhi ama wasimamizi wengine kama Muddyb, Antoni na wengine wengi tu. Miaka kumi na nane ya kusimamia na kutunga makala mbalimbali itakumbukwa hadi mwisho wa dunia ya Wikipedia. Kipala
amechangia
makala za aina mbalimbali ikiwemo, muziki, filamu, tiba, elimu ya nyota, dini, siasa, demografia, jiografia, sayansi, na mengine mengi. Amepata kuwa msaada mkubwa kwa wachangiaji wapya kutoka sehemu mbalimbali za dunia. Alianzisha Jenga Wikipedia ya Kiswahili kwa lengo la kuboresha makala mbalimbali na kutoa mafunzo kwa watu wapya. Pengo lake halitazibika. Sisi wanajumuia ya Wikipedia ya Kiswahili tunasikitika kutangaza kifo chake!
|
|
Takwimu ya Wikipedia ya Kiswahili
- Idadi ya makala:
80,828
- Idadi ya kurasa zote:
174,260
(pamoja na kurasa za watumiaji, majadiliano, msaada n.k.)
- Idadi ya hariri:
1,332,438
- Idadi ya watumiaji waliojiandikisha:
67,124
- Idadi ya
wakabidhi
:
17
- Idadi ya watumiaji hai:
196
(Watumiaji waliojiandikisha na kuchangia katika muda wa siku 30 zilizopita)
- Bofya hapa kwa kupata namba za sasa
- Katika
mwezi wa Agosti 2020
wikipedia ya Kiswahili iliangaliwa mara milioni 1.73 hivi, ambayo ni sawa na mara 55,800 kwa siku au mara 2,326 kila saa. Asilimia 52 za wasomaji wetu wako Tanzania, asilimia 13 wako Kenya, asilimia 18 wako Marekani na mnamo asilimia 10 wako Ulaya.
- Angalia idadi ya wasomaji kwa makala mbalimbali
- (fungua anwani kwa browser yako, ondoa majina yaliyopo na ingiza jina la makala (hadi makala 10) unayopenda. Unaweza kubadilisha kipindi cha taarifa utakachoona; takwimu kabla ya 2015
hapa
)
- na makala 100 zilizotazamiwa zaidi
"Topviews"
kwa kipindi fulani.
- (unachagua kati ya makala 100 kwa mwezi au kwa siku)
Michango ya wanawiki:
angalia hapa michango ya mtumiaji kwenye kila mradi wa Wikimedia
(
andika jina la mtumiaji kwenye sanduku
)
Jumuia za Wikimedia
Kamusi elezo ya Wiki ni kamusi elezo huru iliyo chini ya
Shirika Lisilo la Kiserikali
la
Wikimedia Foundation
, ambalo linasimamia miradi mingine mbalimbali ambayo imeorodheshwa hapo chini. Mpaka sasa miradi inayopatikana Kiswahili ni Wikipedia na Wikamusi. Wikitabu imewekwa Kiswahili lakini bado ni tupu. Mengine inapatikana Kiingereza pamoja na lugha tofauti.
Wikipedia kwa lugha nyingine
Wikipedia kwa lugha nyingine
|
|