Wadominiko
ni jina fupi linalotumka kuhusu wafuasi wote wa
Dominiko wa Guzman
(
1170
-
1221
), hasa wa
Shirika la Ndugu Wahubiri
alilolianzisha, mojawapo kati ya mashirika ya
kitawa
ya
Kanisa Katoliki
, aina ya
Ombaomba
. Ufupisho wa jina la shirika ni
O.P.
Shirika lilianzishwa na
Dominiko wa Guzman
,
mkanoni
wa
jimbo
la
Burgo de Osma-Ciudad de Osma
: mwaka
1203
aliongozana na
askofu
wake
Diego wa Acevedo
katika safari ya kibalozi kwa niaba ya
mfalme
Alfonso VIII wa Castilia
kwa mfalme
Valdemaro II wa Denmark
. Wakati wa kurudi, wakipitia mkoa wa
Langadoque
(
Ufaransa
Kusini), waling'amua
uzushi
wa
Wakatari
ulivyoenea naye akaamua kuungana na mabalozi wa
Papa Inosenti III
katika jitihada za kurudisha watu hao katika
Kanisa Katoliki
.
Akikusanya kundi dogo la wasichana walioacha Ukatari, maka
1207
alianzisha huko Notre-Dame-de-Prouille, karibu
Fanjeaux
,
monasteri
ya kike ambayo ikawa kitovu cha kazi yake ya kitume.
Dominiko aliendelea kuwahubiri kwa amani Wakatari hata baada ya
balozi
wa
Papa
Petro wa Castelnau
kuuawa (
1208
), akikataa kujiunga na
vita vya msalaba
vilivyotangazwa dhidi ya Wakatari.
Kwa msaada wa askofu wa
Tolosa
Folco, mwaka
1215
alikusanya wenzi kadhaa wenye nya ya kuhubiri kama yeye akawaingiza katika
maisha ya kitawa
: shirika hilo lilipata kwanza kibali fulani cha
Papa Inosenti III
halafu kibali rasmi cha mwandamizi wake,
Papa Onori III
, tarehe
22 Desemba
1216
.
Baada ya hapo Shirika la Ndugu Wahubiri lilienea kati
Ulaya
nzima, hasa katika miji ambapo vilikuwa vinaanza
vyuo vikuu
, kama vile vya
Bologna
na
Paris
, vilivyosaidiwa sana na Wadominiko kupata ustawi.
Kwa agizo la
Mtaguso IV wa Laterano
ndugu hao walipaswa kujichagulia
kanuni
iliyowahi kukubaliwa na
Kanisa
, wakaamua kushika ile ya
Agostino wa Hippo
, wakiiongezea
katiba
ya kwao, maarufu hasa kwa kutumia kiasi fulani cha
demokrasia
, ambayo ilitumiwa kama mwongozo kwa nyingine hata za kiserikali.
Ni hasa ile ya kuhubiri, ambayo wakati ule ilikuwa ya nadra, kutokana na hali ya elimu hata kati ya ma
kasisi
. Utume huo, uliokubaliwa na Papa kwa wanashirika wote, ukawa msaada mkubwa kwa Kanisa pia kwa sababu uliendana na maisha ya
ufukara wa Kiinjili
.
Mambo muhimu ya shirika ni:
- Kuhubiri
Injili
- Kuishi kijumuia
- Kuadhimisha
liturujia
- Kushika taratibu za kitawa
- Kusoma
Tarehe
31 Desemba
2005
, Shirika lilikuwa na
konventi
615 zenye ndugu 6.077, ambao 4.495 kati yao ni
mapadri
. Mbali ya hao, kuna
masista
wengi wa maisha ya sala tu na wa maisha ya sala na utume. Pia kuna
walei
wanaofuata
karama
ya shirika hilo katika maisha ya kawaida.