Ubuddha
ni mfumo wa kidini uliotokana na mafundisho ya
Siddharta Gautama
aliyejulikana kama
Buddha
.
Kuna wafuasi wengi, hasa katika
Asia
ya Kusini, Kusini-Mashariki na Mashariki. Makadirio ya idadi yao ni kati ya milioni 488-535 (7-8% ya watu wote duniani). Hivyo ni
dini
kubwa ya nne baada ya
Ukristo
,
Uislamu
na
Uhindu
.
Mafundisho yao yalianzishwa na Siddhartha Gautama aliyezaliwa mnamo mwaka
563 KK
kufuatana na
mapokeo
; wataalamu wengine huona ya kwamba alizaliwa
karne
moja baadaye.
Wanahistoria wengi wa mwanzo wa
karne ya 20
walitaja miaka
563 KK
hadi
483 KK
hivi,
[1]
lakini maoni ya siku hizi yanataja mwaka wa kufariki kati ya
486 KK
na 483 KK au, hata kati ya
411 KK
na
400 KK
.
[2]
[3]
Kadiri ya
akiolojia
, Buddha aliweza kuzaliwa huko
Lumbini
, (leo nchini
Nepal
)
[4]
[5]
[4]
au huko
Kapilavastu
,
Piprahwa
,
Uttar Pradesh
,
India
au tena
Kapileswara
,
Orissa
,
India
.
[6]
[7]
[8]
[9]
[10]
Anaitwa pia "Buddha wa kihistoria" au "Buddha Shakyamuni" kwa sababu katika
imani
yao kuna mabuddha mbalimbali.
Neno "Buddha" si
jina
bali
cheo
cha heshima chenye maana ya "aliyeamka". Humo mna kiini cha imani ya Ubuddha kuwa
binadamu
huishi kwa kawaida bila ya kutambua hali yake mwenyewe, lakini akielewa mafundisho anakuja kuamka na kuona hali yake pamoja na
njia
inayopaswa kufuatwa.
Katika haya yote Wabuddha hufuata mfano wa Buddha Shakyamuni wakitegemea kufika kwenye hali ya kuamka.
Kati ya Wabuddha kuna mielekeo mbalimbali kama
madhehebu
. Yale yenye wafuasi wengi ni:
Maisha na mafundisho ya Gautama Buddha
[
hariri
|
hariri chanzo
]
Yeye alizaliwa na kupewa jina la Siddharta kutoka kwenye
familia
ya kifalme ya
ukoo
wa Shakyamuni yapata miaka 2500 iliyopita huko
India
ya kaskazini.
Mama
wa Buddha alifariki angali yeye ni mtoto na tena alikuwa na shauku la kuwa mtoto atayemzaa si wa kawaida. Akiwa
mjamzito
, aliota
ndoto
ya
tembo
mweupe aliyehusunika na mtoto atakayejifungua.
Jambo hilo lilikuwa
dalili
ya kwamba
mtoto
atakayezaliwa atakuwa mtu mwenye
bahati
, tena maalum.
Mwona aliyetembelea
jumba la kifalme
ili kutoa
utabiri
wake kuhusu maajaliwa ya mtoto, kwa mujibu wa
desturi
na
mila
za siku zile, alitabiri kwamba mtoto huyo atakuja kuwa mkubwa na
mtawala
mahiri; ama ataiacha
kasri
ya
baba
yake na kuishi
maisha ya upwekeni
kutafuta
shauri
kuu kuhusu
Maisha
na
Uhai
.
Baba yake Siddharta aliyekuwa
mtawala
, alishtushwa mno na
kauli
juu ya mtoto wake kuja kuwa
Mmistiya
. Hivyo alijitahidi kila aliloweza kumficha mtoto kuhusu upande wa maisha wenye sura ya
tabu
na ma
hangaiko
. Akijaribu kumsogezea na kumpa kila
fahari
ya maisha ili asahau sehemu ya
nafsi
yake yenye uwezekano wa kumfanya aghairi maisha ya
anasa
ili kwenda kuishi ki
maskini
kama wamistiya wengi wa
zama
zile walivyokuwa wakifanya, kutoka mijini na kwenda
porini
kuishi maisha duni na hali ya asili.
Alipofikia
umri
wa kuoa, baba yake alimpa
mke
ambaye alimzalia
mjukuu
mmoja. Hapo Siddharta alikuwa anatimiza miaka takribani ishirini na tisa.
Safari nne za Siddharta nje ya jumba la kifalme
[
hariri
|
hariri chanzo
]
Wakati ule Siddharta alitoka nje ya jumba la kifalme la baba yake kwa mara ya kwanza akiongozana na
mtumishi
wake mmoja mwadilifu.
Alishangaa sana alipomwona
mtu
aliyetembea kwa
shida
tu na
uso
ulikuwa na ma
finyo
. Akamwuliza mtumishi wake, "Kwa nini mtu huyu anatembea kwa shida na uso wake unaonyesha mafinyo?" Mtumishi akamjibu, "Huyu ni
mzee
. Watu wote watakuwa wazee siku mmoja. Ni hali ya kawaida". Siddharta, asiyewahi kumwona mzee kwa sababu baba yake hakuruhusu wazee katika
mazingira
ya mtoto wake, akashtuka akauliza: "Je, na mimi nitakuwa mzee na nitaonekana hivyo?". Mtumishi akamjibu, "Ndiyo, na wewe utazeeka kama kila mtu." Wakarudi kwao
kimya
.
Wakatoka nje tena.
Safari
ya pili wakamwona
mgonjwa
, na safari ya tatu wakaona
maiti
. Kila safari Siddharta alisikia ya kwamba hata yeye ataona mambo hayo maishani mwake. Yote yalimgusa sana akawa na
wasiwasi
kwa sababu pande hizo za maisha ziliwahi kufichwa mbele yake.
Katika safari ya nne walimwona
mtawa
wa
Kihindu
aliyeketi kando ya
barabara
. Siddharta alivutwa sana na
fikra
ya kwamba mtu huyO aliachana na
mali
na mambo yote kwa
hiari
yake na kufikia
uhuru wa roho
na hakuogopa tena
kifo
.
Hapo alikata shauri moyoni mwake kuondoka katika maisha ya kifalme na kutafuta maisha ya
utawa
.
Siddharta aliondoka nje ya jumba la kifalme
usiku
mmoja bila ya kumwaga mtu yeyote, akajiunga na kundi la watawa na kufuata maisha yao.
Hatimaye, akiwa na wenzake alikutana nao katika
harakati
zake kutafuta
kilele
cha
ufahamu
, walikwenda kuishi kwenye misitu ya mbali na kudumu katika
kutafakari
na Milaya.
Miaka sita ilipita, iliyojaa maisha ya kujima na kila namna ya kuusonga
mwili
ili kutafuta
taamuli
. Hatimaye Siddharta mtawa alidhoofu na
mwili
wake kukonda kutokana na
kufunga
kwa siku mfululizo.
Siku moja akiwa mwenye kukata tamaa, akiwa kando ya
mto
, alipita
mwanamke
aliyebeba
maziwa
. Siddharta alimwomba yule mwanamke ampatie maziwa anywe, maana alikuwa mwenye kuhitaji. Basi yule mwanamke akampatia. Baada ya kunywa na kushukuru alijisikia ni mwenye
utulivu
akajisemea
moyoni
kwamba baada ya hapo ataketi chini ya
mti
na hatainuka tena mpaka atapotokewa na Taamuli.
Huo ukawa mwanzo mpya uliofuatiwa na
baraka
na
neema
. Kwani ni usiku uliofuatia alitokewa na Taamuli na
Ufunuo
. Katika
imani
ya Wabuddha akabadilika kuwa "Buddha" katika usiku huo yaani mtu aliyepokea
ufunuo
na
ujuzi
.
Baada ya hapo alikaa na kutafakari mambo yote aliyoyaona na kuangalia jinsi atakavyoweza kufundisha
njia
yenye kuleta
wongofu
. Kwani Taamuli yake ilifuatia kutambua
Kweli Nne
kuhusu maisha.
Baadaye alifundisha huko na huko India mashariki, kama vile
Magadha
na
Ko?ala
.
[11]
[12]
Kweli
ya Kwanza ni kuwa Maisha ya duniani ni
mateso
kutoka kuzaliwa hadi kufa, hata
kifo
si mwisho kwani maisha ni
mzunguko
wa
majira
ya kufa na kuzaliwa tena na tena.
Kweli ya Pili ni kuwa
asili
ya masumbuko yote ni
Ujinga
, yaani kutokujua namna asilia na
kanuni
ya mambo na hali za maisha na jinsi yanavyosonga.
Kweli ya Tatu ni kwamba shida na masumbuko hutokana na kujishikiza kwa mwanadamu na mambo ya dunia hii pasipo uelewa wa lolote linalozidi
milango ya fahamu
na budi (Sehemu ya Akili yenye kuendesha fikra kutokana na milango ya fahamu).
Kweli ya Nne ni kwamba njia ya
wongofu
yaani namna ya kutoka katika ma
tatizo
hayo aliyoiita (Njia ya Nguzo Nane).
Ni
gurudumu
la
nguzo
nane ambazo humuongoza mwanadamu kuelekea kwenye Taamuli na hasa kufikia wongofu. Kufikia wongofu ni kuachana na
mzunguko wa kufa na kuzaliwa
unaosababishwa na matakwa yenye msingi wa Budi inayojengeka na kurudisha hali za kimaisha zenye kufanya
mzunguko usiokoma
wa masumbuko. Hivyo, njia hii iliyoitwa Dhammapada (Dhamma ni
uadilifu
na Pada ni njia) ndiyo pekee yenye kumkomboa mwanadamu kutoka kwenye taabu na masumbuko ya
ulimwengu
. Nayo ina nguzo nane zifuatazo.
Moja ni
Ono
sahihi.
Pili ni
Dhamira
sahihi.
Tatu ni
Kauli
sahihi
Nne ni
Jitihada
sahihi.
Tano ni
Tendo
sahihi.
Sita ni
Isho
sahihi.
Saba ni
Umakini
sahihi.
Nane ni
Mkazo nia
sahihi.
Mkazo nia ni
dhana
ya kudumu katika kitendo cha
akili
yenye kuona pasipo kusogea ama kutangatanga juu ya jambo moja hadi lingine. Na hii ndio
kigezo
kikuu cha Siddhaharta Buddha katika kufundisha Milaya yenye kuongoza kwenye Taamuli.
Vipassana
.
- ↑
L. S. Cousins (1996), "
The dating of the historical Buddha
Archived
26 Februari 2011 at the
Wayback Machine
.: a review article",
Journal of the Royal Asiatic Society
(3)6(1)
: 57?63.
- ↑
See the consensus in the essays by leading scholars in
The Date of the Historical ??kyamuni Buddha
(2003) Edited by A. K. Narain. B. R. Publishing Corporation, New Delhi.
ISBN 81-7646-353-1
.
- ↑
"If, as is now almost universally accepted by informed Indological scholarship, a re-examination of early Buddhist historical material, ..., necessitates a redating of the Buddha's death to between 411 and 400 BCE...." ?Paul Dundas,
The Jains
, 2nd edition, (
Routledge
, 2001),
p. 24.
- ↑
4.0
4.1
"Lumbini, the Birthplace of the Lord Buddha"
. UNESCO
. Iliwekwa mnamo
26 Mei
2011
.
- ↑
"Nakala iliyohifadhiwa"
. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka
chanzo
mnamo 2012-10-31
. Iliwekwa mnamo
2015-01-21
.
- ↑
"Kapilavastu"
. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka
chanzo
mnamo 2011-01-08
. Iliwekwa mnamo
1 Machi
2011
.
- ↑
"Nakala iliyohifadhiwa"
. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka
chanzo
mnamo 2013-06-03
. Iliwekwa mnamo
2015-01-21
.
- ↑
http://www.rediff.com/news/2002/sep/16spec.htm
- ↑
http://www.srilankaguardian.org/2008/03/buddha-born-in-orissa-scholars.html
- ↑
"Nakala iliyohifadhiwa"
(PDF)
. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka
chanzo
(PDF)
mnamo 2012-03-18
. Iliwekwa mnamo
2015-01-21
.
- ↑
Warder, A.K.
Indian Buddhism
. 2000. p. 45
- ↑
Skilton, Andrew.
A Concise History of Buddhism.
2004. p. 41