Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Georgi Konstantinovich Zhukov
(1 Desemba
1896
- 18 Juni
1974
) alikuwa
jenerali
wa
Umoja wa Kisovyeti
. Wakati wa
Vita Kuu ya Pili ya Dunia
aliongoza
Jeshi Jekundu
hadi
ushindi
wake juu ya
Ujerumani
ya
Adolf Hitler
. Baada ya
vita
aliendelea kuwa
Waziri wa Ulinzi
na mwanachama wa
Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti
.
Zhukov alizaliwa katika
familia
ya
wakulima
maskini
[1]
kwenye
Kaluga Oblast
ya
Urusi ya Magharibi
wakati wa
utawala
wa kifalme. Alipokuwa
kijana
alipaswa kuingia katika
jeshi
la
Urusi
. Wakati wa kuporomoka kwa jeshi hilo katika
mapinduzi ya Kirusi
alijiunga na Jeshi Jekundu
[2]
alipoendeelea kupanda ngazi.
Baada ya kipindi cha mtakaso wa kisiasa chini ya
Josef Stalin
maafisa wengi wa jeshi waliuawa au kufukuzwa, Zhukov aliweza kuingia haraka katika ngazi ya juu.
Alitumwa
Mongolia
alipoongoza Jeshi Jekundu dhidi ya uvamizi wa
Japani
na kushinda maadui
[3]
.
Baada ya uvamizi wa Ujerumani katika Umoja wa Kisovyeti, aliongoza utetezi wa
Leningrad
,
Moscow
, na
Stalingrad
[4]
. Kwenye mwisho wa vita aliongoza vikosi vilivyoteka
Berlin
alipopokea majenerali Wajerumani waliosalimisha amri mnamo 9 Mei
1945
.
Baada ya vita alikuwa gavana wa kijeshi katika
Ujerumani ya Mashariki
kwa muda mfupi halafu alishushwa cheo na Stalin aliyeogopa umaarufu wake
[5]
. Mwaka 1953 alirudi Moscow wakati wa kifo cha Stalin na uongozi mpya ulimpa uwaziri wa ulinzi
[6]
; alipokelewa pia katika kamati kuu ya chama.
Mnamo 1957 alishtakiwa kuwa na uhusiano wa karibu mno na
jenerali Eisenhower
wa Marekani alipaswa kustaafu.
Mnamo 1958 alianza kutunga wasifu zake lakini chama cha kikomunisti iliingila kwa kudai mabadiliko. Sehemu za wasifu zilitolewa miaka mingi baada ya kido chake na baada ya mwisho wa Ukomunisti nchini Urusi.
Mwaka 1968 alipigwa mara ya kwanza na upoozaji akaaga dunia baada kupooza mara ya pili mwaka 1974.
Zhukov alipokea heshima nyingi kwa mafanikio yake ya kijeshi akikumbukwa kama shujaa wa kitaifa.
- ↑
Герои Страны
- ↑
Kigezo:In lang
B. V. Sokolov (2000)
В огне революции и гражданской войны
, in
Неизвестный Жуков: портрет без ретуши в зеркале эпохи
, Minsk: Rodiola-plus.
- ↑
Coox, A. D. (1985). Nomonhan: Japan Against Russia, 1939. Stanford University Press. ISBN 9780804711609.
- ↑
Zhukov, G. K. (2003). Memories and Reflections (in Russian). 2. Moscow: Olma Press. ISBN 9785224031979.
- ↑
Spahr, W. J. (1993). Zhukov: The Rise and Fall of a Great Captain. Novato: Presidio Press. ISBN 9780891414698.
- ↑
Associated Press, 9 February 1955, reported in
The Albuquerque Journal
p. 1.
Wikimedia Commons ina media kuhusu: