Afrika Kusini
ni nchi kubwa ya
Afrika ya Kusini
yenye wakazi takriban
milioni
54.
Republic of South Africa
Afrika Kusini
Majina mengine kwa lugha rasmi 10
[1]
|
Kaulimbiu ya taifa:
/Xam
:
!ke e:
?
xarra
?
ke
(
Kiswahili
: "Umoja katika utofauti" au kifasihi, "Umoja wa watu tofauti")
|
Wimbo wa taifa
:
National anthem of South Africa
|
|
Mji mkuu
|
Cape Town
(
Bunge
)
Pretoria
(
Serikali
)
Bloemfontein
(
Mahakama Kuu
)
33°55′?S 18°25′?E
|
Mji?mkubwa?nchini
|
Johannesburg
|
Lugha?rasmi
|
Kiafrikaans
,
Kiingereza
,
Kizulu
,
Kixhosa
,
Kiswati
,
Kindebele
,
Kisotho cha Kusini
,
Kisotho cha Kaskazini
,
Kitsonga
,
Kitswana
,
Kivenda
|
Serikali
|
Jamhuri
Cyril Ramaphosa
|
Uhuru
Muungano wa Afrika Kusini
|
31 Mei
1910
|
Eneo
?- Jumla
?- Maji (%)
|
1,221,037?km²
?(ya 25)
kidogo sana
|
Idadi ya watu
?-
Julai 2005
kadirio
?-
2014
sensa
?- Msongamano wa watu
|
47,432,000
[1]
(ya 25)
54,002,000
42.4/km² (ya 169)
|
Fedha
|
Rand
(
ZAR
)
|
Saa za eneo
?- Kiangazi?(
DST
)
|
(
UTC
+2)
not observed (
UTC
+2)
|
Intaneti TLD
|
.za
|
Kodi ya simu
|
+27
-
|
1.)
angalia:
Makadirio ya idadi ya watu ni pamoja na vifo kutokana na
UKIMWI
.
|
Imepakana na
Namibia
,
Botswana
,
Zimbabwe
,
Msumbiji
na
Uswazi
. Nchi nzima ya
Lesotho
iko ndani ya eneo la Afrika Kusini.
Mji mkubwa
ni
Johannesburg
. Majukumu ya
mji mkuu
yamegawiwa kati ya miji mitatu:
Cape Town
ni makao ya
Bunge
,
Pretoria
ni makao ya
Serikali
na
Bloemfontein
ni makao ya
Mahakama Kuu
.
Jina
Nchi ina majina rasmi 11 kutokana na
lugha rasmi
11, nazo ni:
Kiafrikaans
,
Kiingereza
,
Kizulu
,
Kixhosa
,
Kiswati
,
Kindebele
,
Kisotho cha Kusini
,
Kisotho cha Kaskazini
,
Kitsonga
,
Kitswana
na
Kivenda
.
Historia
Zamadamu waliishi katika eneo la Afrika Kusini tangu miaka milioni 3 iliyopita, inavyoshuhudiwa na
akiolojia
.
Binadamu
wameishi huko kwa miaka 170,000 mfululizo. Wakazi wa muda mrefu zaidi ni
Wakhoikhoi
na
Wasani
, ambao wazagumzumza lugha ya
jamii
ya
Khoi-San
.
Katika
karne ya 4
au
ya 5
walifika
Wabantu
ambao waliwazidi nguvu hao wa kwanza.
Koloni la Waholanzi kwenye Rasi
Chanzo cha Afrika Kusini kama nchi ni
Koloni la Rasi
iliyoundwa na
Waholanzi
katika eneo la
Cape Town
kuanzia mwaka
1652
. Huko
kabila
jipya la
Makaburu
lilijitokeza kati ya
walowezi
Wazungu
kutoka
Uholanzi
,
Ufaransa
na
Ujerumani
. Lugha yao ilikuwa
Kiholanzi
iliyoanza kuchukua maneno ya
Kifaransa
,
Kiafrika
na
Kiingereza
na kuendelea kuwa lugha ya pekee
Kiafrikaans
.
Karne za kwanza za koloni la Kiholanzi ziliona pia kufika kwa
watumwa
kutoka
Indonesia
walioletwa kama
wafanyakazi
wa Waholanzi na Makaburu. Hao Waindonesia walikuwa
chanzo
cha
jumuiya
ya
Uislamu
kwenye
rasi
.
Pia
machotara
walitokea kutokana na kuzaliana kati ya Makaburu na
wanawake
Waafrika
na Waindonesia. Sehemu ya machotara hao wameingia katika jumuiya ya Makaburu na wengi wao wanapimwa kuwa na mababu Waafrika.
Katika miaka ya baadaye
ubaguzi wa rangi
uliongezeka na watoto machotara wa Wazungu na Waafrika mara nyingi hawakukubalika; walianza kuishi kama kundi la pekee kati ya Waafrika na Wazungu, nao ni chanzo cha hao walioitwa baadaye "Cape Coloreds".
Milki za Waafrika na Mfecane
Sehemu kubwa ya eneo
kaskazini
kwa rasi ilikaliwa na makabila ya Waafrika.
Mnamo mwaka
1800
falme na milki zilianza kutokea hapa. Mwanzo wa
karne ya 19
ni hasa
Wazulu
chini ya
Shaka Zulu
walioanza kuenea na kuwashambulia majirani katika
vita vya Mfecane
. Vita hivyo vilileta
uharibifu
mkubwa lakini vilisababisha pia kutokea kwa milki za
Wasotho
na
Watswana
na wengine walioiga mitindo ya Wazulu na kujenga ma
dola
yenye uwezo wa ki
jeshi
.
Kuingia kwa Uingereza na jamhuri za Makaburu
Mwaka
1814
Koloni la Rasi lilitwaliwa na Waingereza na kuwa sehemu ya
Milki ya Uingereza
.
Utawala
wa Waingereza ulisababisha
uhamisho
wa nje wa sehemu ya Makaburu waliotokana na Wazungu kutoka Uholanzi, Ufaransa na Ujerumani; Makaburu hao walihama kwenda kaskazini wakaanzisha
jamhuri
ndogo kati ya maeneo ya Waafrika ama kwa njia ya mapatano au kwa njia ya
vita
.
Kati ya miaka
1840
na
1850
Waingereza waliwafuata Makaburu kwa kueneza maeneo yao hadi
mto Oranje
; waliteka jamhuri ya Kikaburu ya
Natalia
na kuanzisha koloni jipya la
Natal
.
Jamhuri mbili za Makaburu ziliweza kustawi kwa miaka kadhaa ambazo zilikuwa jamhuri ya
Dola Huru la Oranje
upande wa kaskazini wa mto Oranje na jamhuri ya
Transvaal
(ilijiita pia Jamhuri ya Kiafrika ya Kusini) upande wa kaskazini wa
mto Vaal
.
Waafrika, Waingereza na Makaburu waligongana
Milki za Kiafrika zilitafuta njia zao kati ya
himaya
hizi za Wazungu ambao walikuwa na nguvu kutokana na
silaha
za kisasa. Wengine walitafuta
uhusiano
mzuri na Makaburu na kushikamana nao; wengine waliona Makaburu kama
hatari
wakatafuta uhusiano wa
ulinzi
na Waingereza.
Mikataba kati ya Waingereza na milki za Kiafrika iliunda
nchi lindwa
zinazoendelea hadi leo kama
nchi huru
kama vile
Botswana
(Bechuanaland),
Lesotho
(Basutoland) na
Uswazi
(Swaziland).
Katika
miaka ya 1880
almasi
na
dhahabu
zilipatikana kwa wingi katika jamhuri hizi na kusababisha kufika kwa
wachimbamadini
wengi, hasa Waingereza, waliotaka kutajirika; Makaburu walisita kuwapa
haki za kiraia
kwa sababu waliogopa
wageni
wengi.
Tatizo
hilo lilisababisha vita vya Makaburu dhidi ya Uingereza na jamhuri za Makaburu zilitwaliwa na jeshi la Kiingereza hadi mwaka
1902
zikawa makoloni.
Karne ya 20: Muungano wa Afrika Kusini
Jitihada za kupatanisha Wazungu wa Afrika Kusini (yaani Waingereza na Makaburu) zilisababisha kuundwa kwa
Muungano wa Afrika Kusini
kama
nchi ya kujitawala
ndani ya Milki ya Uingereza. Waafrika kwa jumla hawakuwa na haki za kiraia katika nchi hiyo isipokuwa katika
Jimbo la Rasi
kama walikuwa na elimu na
mapato
ya kulipa
kodi
za kutosha.
Siasa ya Apartheid tangu 1948
Baada ya
vita kuu ya pili ya dunia
Chama cha National kilichofuata
itikadi kali
ilipata
kura
nyingi na kuchukua
serikali
ya Afrika Kusini. Hapo ilianzisha mfumo wa ubaguzi wa rangi kwa jina la
apartheid
.
Haki za wasio Wazungu zilipunguzwa zaidi. Maeneo ya Kiafrika yalitangazwa kuwa nchi za pekee chini ya
usimamizi
wa serikali ya Kizungu ya Afrika Kusini; kwa hiyo wananchi kutoka maeneo hayo hawakuwa tena na haki za kukata
rufaa
mbele ya
mahakama
; walipewa vibali vya muda tu kukaa kwenye miji. Waafrika walipaswa kutembea muda wote na
pasipoti
na vibali;
ndoa
na
mapenzi
kati ya watu wa
rangi
tofauti zilipigwa
marufuku
.
Shule
na
makazi
zilitenganishwa.
Siasa hiyo ilisababisha
farakano
kati ya nchi nyingi za
dunia
na Afrika Kusini.
Upinzani
kutoka Uingereza na
Jumuiya ya Madola
ulisababisha kuondoka kwa Afrika Kusini katika jumuiya hiyo na kutangazwa kwa Jamhuri ya Afrika Kusini.
Afrika Kusini mpya
Mwaka 1990 Apartheid ilikwisha na serikali ya National Party ilipaswa kuendesha
uchaguzi huru
kwa wananchi wote na kukabidhi
madaraka
kwa serikali ya
ANC
chini ya
Nelson Mandela
.
Utawala na muundo wa shirikisho
Miji Mikubwa
Hii ifuatayo ni miji/manispaa/majiji kumi yenye wakazi wengi zaidi nchini.
Na.
|
Manispaa au Jiji
|
Wakazi (2001)
|
Wakazi (1996)
|
Asilimia ya badiliko
1996-2001
|
1.
|
Johannesburg
,
Gauteng
|
3,225,812
|
2,639,110
|
22.2%
|
2.
|
Durban
,
KwaZulu-Natal
|
3,090,117
|
2,751,193
|
12.3%
|
3.
|
Cape Town
,
Rasi ya Magharibi
|
2,893,251
|
2,563,612
|
12.9%
|
4.
|
East Rand
,
Gauteng
|
2,480,282
|
2,026,807
|
22.4%
|
5.
|
Pretoria
,
Gauteng
|
1,985,984
|
1,682,701
|
18.0%
|
6.
|
Port Elizabeth
,
Rasi ya Mashariki
|
1,005,776
|
969,771
|
3.7%
|
7.
|
East London
,
Rasi ya Mashariki
|
701,881
|
682,287
|
2.9%
|
8.
|
Vereeniging
,
Gauteng
|
658,422
|
597,948
|
10.1%
|
9.
|
Bloemfontein
,
Dola Huru
|
645,441
|
603,704
|
6.9%
|
10.
|
Thohoyandou
,
Limpopo
|
584,469
|
537,454
|
8.7%
|
Watu
Afrika Kusini ina mchanganyiko mkubwa wa watu. Waafrika asili ni
asilimia
80.7, Machotara ni 8.8%, Wazungu ni 7.9%, Waasia ni 2.6%.
Lugha mama
zinazotunika zaidi ni: Kizulu (22.7%), Kixhosa (16%), Kiafrikaans (13.5) na Kiingereza (9.6%), lakini hiyo ya mwisho ndiyo inayotumika zaidi kati ya
makabila
mbalimbali na karibu
nusu
ya wananchi wanajua kuiongea.
Wengi (78.8%) ni
Wakristo
wa
madhehebu
mengi sana, hasa ya
Uprotestanti
;
Wakatoliki
ni 6.8%.
Dini
nyingine ni:
Dini za jadi
(4.4%),
Uislamu
(1.6%),
Uhindu
(1%) na
Uyahudi
(0.1%). Asilimia 12.3 ya watu hawana dini yoyote.
Afrika Kusini inaongoza duniani kwa wingi wa watu wenye
VVU
/
UKIMWI
: mwaka
2015
walikuwa milioni 7. Mwaka 2018 silimia 20.4 za watu wenye
umri
wa miaka 15-49 walikuwa na
virusi
hivyo. Ma
yatima
kutokana na
ugonjwa
huo ni 1,200,000.
Uchumi
Ki
uchumi
Afrika Kusini ni nchi yenye pande mbili kabisa.
Sehemu ya uchumi ina hali ya ki
maendeleo
kabisa ikiwa na
viwanda
na
huduma
zinazolingana na hali ya juu kabisa duniani; hali ya maisha ya wananchi waliomo katika sekta hii inalingana na nchi kama
Australia
au
Ulaya magharibi
.
Kwa upande mwingine hali ya maisha ya sehemu kubwa ya wananchi ni
umaskini
kama katika sehemu nyingine za
Afrika
au
Uhindi
wa ma
shambani
. Lakini kwa ujumla hali ya maisha iko juu kuliko nchi nyingi za Afrika.
Sekta muhimu za uchumi ni
migodi
ya kuchimba dhahabu au almasi, viwanda na huduma kama
benki
au
bima
.
Jeshi
Jeshi la Afrika Kusini ina silaha za kisasa kushinda nchi zote za majirani. Uchumi unawezesha nchi kutumia kiasi kikubwa kwa ajili ya jeshi kuliko nchi zote za Afrika kusini kwa
Sahara
.
Afrika Kusini iliwahi kuwa na
silaha za nyuklia
lakini ilizibomoa baada ya mwaka
1993
.
Watu maarufu
Kati ya watu mashuhuri sana wa Afrika Kusini ni:
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo
- A History of South Africa, Third Edition
. Leonard Thompson. Yale University Press. 1 March 2001. 384 pages.
ISBN 0-300-08776-4
.
- Economic Analysis and Policy Formulation for Post-Apartheid South Africa: Mission Report, Aug. 1991
. International Development Research Centre. IDRC Canada, 1991. vi, 46 p. Without ISBN
- Emerging Johannesburg: Perspectives on the Postapartheid City
. Richard Tomlinson, et al. 1 January 2003. 336 pages.
ISBN 0-415-93559-8
.
- Making of Modern South Africa: Conquest, Segregation and Apartheid
. Nigel Worden. 1 July 2000. 194 pages.
ISBN 0-631-21661-8
.
- South Africa: A Narrative History
. Frank Welsh. Kodansha America. 1 February 1999. 606 pages.
ISBN 1-56836-258-7
.
- South Africa in Contemporary Times
.
Godfrey Mwakikagile
. New Africa Press. February 2008. 260 pages.
ISBN 978-0-9802587-3-8
.
- The Atlas of Changing South Africa
. A. J. Christopher. 1 October 2000. 216 pages.
ISBN 0-415-21178-6
.
- The Politics of the New South Africa
. Heather Deegan. 28 December 2000. 256 pages.
ISBN 0-582-38227-0
.
- Twentieth-Century South Africa
. William Beinart. Oxford University Press 2001, 414 pages,
ISBN 0-19-289318-1
Viungo vya nje
|
Makala hii kuhusu maeneo ya
Afrika Kusini
bado ni
mbegu
.
Je unajua kitu kuhusu
Afrika Kusini
kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|