Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Roko wa Montpellier
(
Montpellier
,
Ufaransa
,
1348
hivi -
Voghera
,
Italia
,
16 Agosti
1379
) alikuwa
Mkristo
maarufu kwa kuishi miaka mingi bila makao maalumu. Ndiyo maana kwa kawaida anachorwa amevaa
nguo
za
hija
.
Katika mizunguko yake sehemu mbalimbali alihudumia kishujaa waliopatwa na
tauni
na kuwaponya wengi kwa
mkono
wake wenye
karama
. Huko
Piacenza
mwenyewe aliugua tauni akapona
[1]
.
Miaka 3-5 ya mwisho alikuwa mfungwa
gerezani
akidhaniwa
mpelelezi
, asifanye chochote kwa kujitetea au kujitambulisha kwa
watawala
ambao walikuwa
ndugu
zake wakamtambua baada ya kufa tu.
Tangu kale ni kati ya
watakatifu
maarufu zaidi
duniani
, pia kwa sababu ya
miujiza
iliyosemekana alifanya wakati wa
uhai
wake na baada ya
kifo
, hasa kwa
wagonjwa
wa tauni, kama alivyoahidi kwa
maandishi
.
Sikukuu
yake ni tarehe
16 Agosti
[2]
.
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
|
Makala hii bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuiongezea habari
.
|