Muungano wa Kijerumani
(
Kijerumani
:
Deutsche Wiedervereinigung
, Kiing. German Reunification) ulikuwa mchakato wa kuunganisha sehemu za Ujeruamni zilizowahi kutenganishwa. Muungano huo ulitokea kwenye mwaka 1990 wakati majimbo ya
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Ujerumani
(Ujerumani Mashariki) yalijiunga na Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani (Ujerumani Magharibi).
Baada ya
Vita Kuu ya Pili ya Dunia
, Ujerumani iligawanywa na washindi kwa kanda nne vilivyosimamiwa na Marekani, Urusi, Uingereza na Ufaransa.
1949 Wajerumani walianza tena kujitawala katika nchi mbili. Kanda za
Marekani
,
Uingereza
na
Ufaransa
ziliungana kwa jina la
Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani
liliofuata siasa ya demokrasia ya vyama vingi na uchumi wa kibepari. Kanda la Kirusi lilikuwa
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kijerumani
lililofuata siasa ya utawala wa chama cha kikomunisti na uchumi wa kijamaa.
Hadi mwaka 1960 uchumi wa magharibi umepita ule wa mashariki. Hali ya maisha katika magharibi ilianza kuwa bora na pamoja na udikteta wa kisiasa wa Wakomunisti wananchi wengi wa mashariki walivuka mpaka wakahamia magharibi. Kwa hivyo serikali ya mashariki ilianza kujenga fensi kwenye mpaka na kwenye Agosti 1961 ilijenga
ukuta wa Berlin
uliozuia watu wa mashariki wasiweze tena kufika magharibi.
Hadi mwaka 1989 hali ya kiuchumi katika mashariki ilizidi kubaki nyuma ya magharibi, na kwa jumla uchumi ulikuwa matatani. Wakati ule kiongozi wa Umoja wa Kisoveti
Mikhail Gorbachev
alianza kulegeza ukali wa utawala wa kikomunisti
[1]
. Watu wengi kwenye mashariki hawakuwa tena tayari kunyamaza na idadi ya wakimbizi wa kwenda magharibi iliongezeka kwa ghafla wakipita nchi jirani za kikomunisti kama Chekoslovakia na Hungaria ambako watawala hawakuwa tayari tena kuwazuia
[2]
[3]
. Wakati ule, Wajerumani wengi hawakuamini bado kwamba nchi itaunganishwa tena.
[4]
Hatimaye
mpaka
ulifunguliwa tarehe
9 Novemba
1989
[5]
. Utawala wa Wakomunisti uliporomoka haraka na katika kipindi cha miezi 11 iliyofuata
[6]
, masharti ya muungano yalijadiliwa kati ya Ujerumani Mashariki na Magharibi, Ufaransa, Uingereza, Marekani na Umoja wa Kisovieti.
Mkataba wa Masuluhisho ya Mwisho kuhusu Ujerumani uliotiwa saini na nchi hizo mbili ndani ya Ujerumani na nchi za washindi wa Vita Kuu ulifungua njia kuelekea kuungana tena
[7]
[8]
[9]
.
Tarehe
3 Oktoba
1990, saa 00:01 majimbo matano ya
Brandenburg
,
Mecklenburg-Vorpommern
,
Saxony
,
Saxony-Anhalt
,
Thuringia
na
Berlin
yalijiunga rasmi na Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani. Jamhuri ya Kidemokrasia ya Ujerumani ilikoma kuwepo wakati huu.
- The Unification Treaty (Berlin, 31 August 1990)
website of CVCE (Centre of European Studies)
- Hessler, Uwe,
"The End of East Germany"
,
dw-world.de
, 23 August 2005.
- Berg, Stefan, Steffen Winter and Andreas Wassermann,
"Germany's Eastern Burden: The Price of a Failed Reunification"
,
Der Spiegel
, 5 September 2005.
- Wiegrefe, Klaus,
"An Inside Look at the Reunification Negotiations"
Der Spiegel
, 29 September 2010.
- "Unfriendly, even dangerous"? Margaret Thatcher and German Unification,
Academia.edu
, 2016.
- Problems with Reunification
from the
Dean Peter Krogh Foreign Affairs Digital Archives