Kundi la Mawaziri wa Fedha ishirini na Magavana wa Benki Kuu
(linalojulikana kama
G-20
,
G20
au
Group of Twenty)
ni
kundi
la ma
waziri wa fedha
na
magavana
wa
benki kuu
kutoka nchi zenye
uchumi
mkubwa
duniani
: nchi 20, kuongezea
Umoja wa Ulaya
.
Kwa pamoja, uchumi wa G-20 unajumuisha 85
%
ya
[2]
bidhaa jumla zinazotoka katika nchi
[2]
ulimwenguni, 80% ya
biashara
duniani (pamoja na biashara ya EU ya ndani) na
theluthi
mbili
ya
idadi
ya
watu
duniani
.
[3]
G-20 ni kama
ukumbi
wa ushirikiano na kushauriana kuhusu masuala ya
mfumo wa fedha
wa
kimataifa
. Husoma, kupitia upya, na kukuza majadiliano kati ya nchi muhimu za
viwanda
na
soko
zinazoibukia kuhusu masuala ya sera zinazohusu uendelezaji wa udhibiti wa
fedha
kimataifa, na hutaka kushughulikia masuala ambayo yako juu ya
majukumu
ya shirika lolote.
Kwa G-20 kuongeza nguvu tangu kongamano la
Washington
la
mwaka
2008
,
viongozi
wake walitangaza
tarehe
25 Septemba
2009
, kwamba kundi hilo lingechukua pahala pa
G8
kama
halmashauri
kuu ya kiuchumi ya mataifa tajiri.
[4]
Viongozi wa mataifa wanachama wa G-20 hukutana kila mwaka mara mbili katika
Kongamano la G-20.
Mpangilio
G-20 hufanya kazi bila sekretarieti ya kudumu wala wafanyakazi. Uenyekiti huzunguka kila mwaka kati ya wanachama na huchaguliwa kutoka kwa kambi tofauti za nchi. Mwenyekiti ni mmoja wa memba wa kundi la usimamizi la watatu la zamani, sasa na wenyekiti wa baadaye lifahamikalo kama
Troika
. Mwenyekiti wa sasa huunda sekretarieti ya muda kwa wakati wake, ambayo inaratibu kazi ya kikundi na kupanga mikutano yake. Jukumu la Troika ni kuhakikisha mwendelezo wa kazi za G-20 na usimamizi katika miaka ijayo. Ifuatayo ni orodha ya nchi wenyekiti wa G-20:
[5]
Mwanachama wa 20 ni
Umoja wa Ulaya
ambao unawakilishwa na
Rais wa Baraza la Ulaya
na
Benki Kuu ya Ulaya
Kuongezea wanachama hawa 20, vikao na taasisi zifuatazo, zikiwakilishwa na
maofisa watendaji wakuu
, hushiriki katika mikutano ya G-20:
[6]
Uanachama
Uanachama wa G-20 unajumuisha:
Uanachama hauonyeshi kabisa nchi 19 zenye uchumi mkubwa duniani katika mwaka. Shirika hili linasema:
[7]
“
|
kwa ukumbi kama wa G-20, ni muhimu hasa kwa nchi wanachama kuzuiuwa na kufuata kanuni kuhakikisha kuenda vyema na uendelevu kwa shughuli zake. Hakuna vigezo rasmi vya kujiunga na G-20 na mtungo wa kikundi hiki umekuwa haujabadilika tangu kilipoanzishwa. Kwa kuangalia malengo ya G-20, ilifikiriwa ni muhimu kuwa nchi na kanda zenye umuhimu kwenye mfumo wa fedha wa kimataifa zijumuishwe. Mambo kama vile usawa wa Jiografia and kuwakilishwa kwa umma pia yalichangia pakubwa.
|
”
|
Mataifa yote wanachama 19 ni kati ya
chumi bora 32 kama ilivyo pimwa katika Pato la Taifa kwa bei nomino
katika orodha iliyochapishwa na
Shirika la Fedha la Kimataifa
(IMF) mwaka 2008.
[8]
Nchi ambazo hazijawakilishwa katika G-20 ni
Uswisi
(19),
Norway
(25),
Taiwan
(26),
Iran
(28) na
Venezuela
(31), hata ingawa wako juu ya orodha kuliko baadhi ya wanachama.
Uhispania
(9),
Uholanzi
(16),
Poland
(18),
Ubelgiji
(20),
Uswizi
(22),
Austria
(24),
Ugriki
(27) na
Denmark
(29) wanawakilishwa tu kama memba wa EU, wala si memba kamili. Wakati Pato la Taifa linapimwa kwa
viwango vya nguvu za ununuzi (PPP)
, wanachama wote 19 ni kati ya bora 24 duniani katika mwaka 2008, kulingana na IMF.
[9]
Iran
(17),
Taiwan
(19) na
Thailand
(23) si wanachama wa G-20, huku
Uhispania
(12),
Uholanzi
(19) na
Poland
(20)wakijumuishwa tu katika kipengele cha EU. Hata hivyo, katika orodha ya wastani wa Pato la Taifa, iliyokadiriwa kwa miaka tangu kuundwa kwa kundi hili (1999-2008) kwa viwango vyote vya nomino na vya PPP,
Uhispania, Uholanzi, Taiwan
, na
Poland
tu ndiyo wanaonekana juu ya mwanachama yeyote wa G-20 katika orodha zote mbili mtawalia.
[10]
Mara nyingi inasemekana kwamba G20, ingawa inatoa uwakilishi mpana zaidi kuliko
G8
, haina haki ya kufanya maamuzi yanayoathiri dunia nzima, kwa sababu wanachama wake wanachaguliwa bila kanuni zozote. G20 haina mkataba na mijadala yake si ya faraghani, hivyo kuifanya "taasisi isiyo yakidemokrasia."
[11]
Wakosoaji wanapendekeza mbadala kama vile
Baraza la Usalama wa Kiuchumi
katika
Umoja wa Mataifa
, ambapo wajumbe wanapaswa kuchaguliwa na
Mkutano Mkuu
kufuatia umuhimu wao katika uchumi wa dunia na mchango walio tayari kutoa kwa maendeleo ya uchumi wa dunia.
[12]
Historia
G-20, ambayo ilichukua pahala pa
G-33
, ambayo pia ilikuwa imechukua pahala pa
G22
, ilitajwa katika mkutano wa G7 mjini
Cologne
mnamo Juni 1999, lakini ilianzishwa rasmi katika Mkutano wa
G7
wa mawaziri wa fedha mnamo tarehe 26 Septemba 1999. Mkutano wa uzinduzi ulifanyika mnamo tarehe 15-16 Desemba 1999 mjini
Berlin
. Mwakani 2008
Uhispania
na
Uholanzi
waliongezwa kwa mwaliko wa Ufaransa katika Mkutano wa G-20 wa Viongozi kuhusu masoko ya fedha na Uchumi Duniani.
Mnamo 2006, kaulimbiu ya mkutano wa G-20 ilikuwa "Kujenga na Kuendeleza mafanikio. Masuala yaliyojadiliwa ni pamoja na mageuzi ya ndani ili kufikia "ukuaji endelevu", nishati ulimwenguni na masoko ya rasilimali, 'marekebisho' ya Benki ya Dunia na IMF, na athari za mabadiliko demografiki kutokana na idadi ya wanaozeeka.
Trevor A. Manuel
, Mbunge, Waziri wa Fedha,
Afrika ya Kusini
, alikuwa mwenyekiti wa G-20 wakati wa Afrika ya Kusini ilikuwa mwenyeji wa
Sekretarieti ya
mwaka 2007.
Guido Mantega
, Waziri wa Fedha,
Brazili
, alikuwa mwenyekiti wa G-20 mwaka 2008; Brazili ilipendekeza mazungumzo juu ya ushindani katika masoko ya fedha,
nishati safi
na maendeleo ya kiuchumi na vipengele vya fedha vya ukuaji na maendeleo. Katika taarifa kufuatia mkutano wa G7 mawaziri wa fedha tarehe 11 Oktoba 2008, Rais wa Marekani
George W. Bush
alisema kuwa mkutano ujao wa G-20 utakuwa muhimu katika kutafuta jawabu la (uliyoitwa kwa wakati huo)
mgogoro wa kiuchumi
wa 2008. Mpango wa Rais wa Ufaransa
Nicolas Sarkozy
na Waziri Mkuu wa Uingereza
Gordon Brown
ulipelekea kuweko kwa mkutano maalum wa G-20,
Kongamano la Viongozi wa G-20 kuhusu masoko ya fedha na uchumi wa dunia
, mnamo tarehe 15 Novemba 2008.
[13]
Viongozi wa G20 walikutana tena mjini
London
mnamo tarehe 2 Aprili 2009.
[14]
Kongamano lingine la G20 yalifanyika mnamo 24-25 Septemba 2009 mjini
Pittsburgh, Pennsylvania.
[15]
Mikutano ya G-20
Kongamano la G-20 lilianzishwa kama itikio kwa
tatizo
wa
kifedha la 2007-2010
na pia kwa kuonekana kwamba
nchi zinazostawi
hazikuwa zimejumuishwa vya kutosha katika majadiliano ya kiuchumi duniani na utawala. Makongamano ya G-20 ya
wakuu wa nchi
au
serikali
yalifanyika mbali na Mikutano ya G-20 ya Mawaziri wa Fedha na Magavana wa Benki Kuu ambao waliendelea kukutana kuandaa Kongamano la wakuu wa nchi na pia kutekeleza maamuzi yao.
Mikutano ya Mawaziri wa Fedha na Magavana wa Benki Kuu:
Mmenyuko wa Umma
Tangu mwaka 1999, G-20 mikutano mingi ya G-20 imekuwa ikipingwa. Maandamano mengi huanza kwa amani, lakini mingi hugeuka vurugu na watu wengi hujeruhiwa na uharibifu wa mali katika maeneo ya mitaa.
[20]
Sababu hasa za maandamano hubadilika kutoka mkutano hadi mwingine, na hata maandamano mengi wakati wa mkutano mmoja. Hata hivyo, hisia tele na kuguna kwa waandamanaji hakujabadilika. Kama ilivyodhahiri,ukweli ni kwamba maandamano hayo yamekuwa yakiendelea tangu mwaka 1999, na yamendelea kuisha kwa vurugu. Habari zaidi kuhusu maandamano ya mikutano hasa inaweza kupatikana kwenye kurasa za mikutano hiyo katika sehemu ya Angalia Pia.
Angalia Pia
Maelezo
- ↑
FAQ #5: What are the criteria for G-20 membership?
Archived
6 Mei 2013 at the
Wayback Machine
. from the official G-20 website
- ↑
2.0
2.1
"No Clear Accord on Stimulus by Top 20 Industrial Nations."
The New York Times,
ukurasa A1, 15 Machi 2009.
- ↑
Uanachama wa G-20
Archived
4 Mei 2011 at the
Wayback Machine
. kutoka tovuti rasmi ya G-20
- ↑
"
Officials: G-20 to supplant G-8 as international economic council
", CNN, 2009-09-25. Retrieved on 2009-09-25.
- ↑
"Nakala iliyohifadhiwa"
. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka
chanzo
mnamo 2011-05-04
. Iliwekwa mnamo
2010-01-21
.
- ↑
Hitilafu ya kutaja: Invalid
<ref>
tag; no text was provided for refs named
g20members
- ↑
FAQ # 5: Je, nini vigezo vya uanachama wa G-20?
Archived
6 Mei 2013 at the
Wayback Machine
. kutoka tovuti rasmi ya G-20
- ↑
World Economic Outlook Database-Oktober 2008, Shirika la Fedha la Kimataifa.
- ↑
World Economic Outlook Database, Aprili 2009,
Shirika la Fedha la Kimataifa
- ↑
GDP (Nominal).
GDP (PPP)
World Economic Outlook Database, Aprili 2009,
Shirika la Fedha la Kimataifa
- ↑
G20 yapaswa kuongezwa hadi Bilioni 6
Archived
21 Januari 2010 at the
Wayback Machine
. Daniele Archibugi, Opendemocracy.net
- ↑
Baraza la uchumi na Usalama wa Jamii la Umoja wa Mataifa
Frances Stewart na Sam Daws, Oxford University, Machi 2001
- ↑
Kongamano la G-20: je, linahusu nini?,
Kutoka
Taasisi ya Brookings
- ↑
Uingereza kuwa wenyeji wa mkutano G-20 wa kifedha "Novemba
Archived
2008-12-09 at the
UK Government Web Archive
26, 2008 kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu wa Uingereza
- ↑
Marekani kuwa mwenyeji wa mkutano wa G20 unaofuata
BBC News, 28 Mei 2009
- ↑
16.0
16.1
16.2
Kongamano la viongozi wa G-20 kuhusu Masoko ya hisa na Uchumi Duniani
kutoka senta ya habari za G-20 I katika
Chuo Kikuu cha Toronto
- ↑
Kanada kuwa mwenyeji wa kongamano 'mpito' la mwaka 2010
- ↑
"
Korea to Host G20 in November
", The
Korea Times
, 25 Septemba 2009. Retrieved on 26 Septemba 2009.
- ↑
Pointi ya 31 kutoka tamko la viongozi katika kongamano la Pittsburgh 2009
Archived
14 Mei 2011 at the
Wayback Machine
.
- ↑
historia ya maandamano na vurugu katika mikutano ya biashara duniani ya G20
Times Online, 21 Machi 2009
Viungo vya nje
Wikimedia Commons ina media kuhusu: