Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Martiniani, Saturiani na wenzao
wawili walikuwa wote
ndugu
; ni kati ya
wafiadini
wa
Kanisa Katoliki
waliouawa kikatili sana na
Wavandali
katika
karne ya 5
, wakati wa
utawala
wa
mfalme
Genseriki
aliyekuwa
Mwario
.
Wote waliongokea
Ukristo
kwa njia ya
Masima bikira
,
mtumwa
mwenzao.
Baada ya kutoroka, walijiunga na
monasteri
huko Thabraca, lakini walikamatwa na kuuzwa tena.
Huko walikopelekwa (Caprapicta) walivuta wengi katika Ukristo wa
Kikatoliki
[1]
, jambo lililosababisha
chuki
ya Waario hadi wakauawa pengine pamoja na wenzao 361, wakiwemo Saturnini, Nerei na Serea
[2]
.
Habari zao zimeandikwa na
askofu
Vikta wa Vita
.
Tangu kale wanaheshimiwa kama
watakatifu
.
Sikukuu
yao huadhimishwa
tarehe
16 Oktoba
[3]
[4]
[5]
[6]
.
|
Makala hii bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuiongezea habari
.
|