Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Guyane
Lagwiyann
|
|
|
Jina la Kifaransa
|
Guyane
(
kwa Krioli:
Lagwiyann)
|
Jina la kawaida
|
Guyani ya Kifaransa
|
Mji Mkuu
|
Kayeni
|
Eneo
|
86 504 km²
|
Mkuu wa Mkoa
|
Gabriel Serville
|
Idadi ya wakazi
|
301 099
|
Sensa ya mwaka
|
2022
|
Wakazi kwa km²
|
3.2
|
Wilaya (arrondissements)
|
3
|
Ramani
|
|
-- Kwa nchi jirani angalia makala
Guyana
--
Guyani ya Kifaransa
(kwa
Kifaransa
:
Guyane francaise
au
Guyane
tu, kwa
Krioli ya Guyani ya Kifaransa
Lagwiyann
) ni
eneo la ng'ambo la Ufaransa
(
"departement d'outre-mer" au DOM
) katika
Amerika Kusini
.
Makao makuu
ya Guyana ni
mji
wa
Kayeni
.
Imepakana na
Brazil
na
Surinam
.
Pwani
ya
Bahari ya Karibi
(
Atlantiki
) iko upande wa
kaskazini
.
Eneo la Guyani ni mojawapo ya mikoa tisa ya nje zaidi (OR) ya
Umoja wa Ulaya
. Ni eneo pekee la bara la Ufaransa na Umoja wa Ulaya huko Amerika Kusini na eneo la mwisho la Ufaransa katika bara la Amerika.
Ilikuwa
koloni
la
Ufaransa
; sasa imekuwa sehemu kamili ya Ufaransa kisiasa na kisheria. Wakazi ni
raia
wa Ufaransa. Eneo lina hali ya mkoa (fr:departement) na pia kanda (fr:region) katika Ufaransa. Hivyo Guyani ni sehemu ya Umoja wa Ulaya.
Pesa
yake ni
Euro
.
Watu
Idadi
ya wakazi imekadiriwa kuwa 296,711 katika mwaka
2019
na inaendelea kuongezeka kwa
uzazi
na
uhamiaji
.
Wakazi walio wengi ni wa asili ya
Afrika
au
machotara
wa mchanganyiko wa Kiafrika-Kizungu (Wakrioli) (60-70%). Asilimia 14 ni
Wazungu
, hasa kutoka Ufaransa; wengine ni
Waindio
asilia (3-4%),
Wachina
(3-4%),
Wahindi
na
wahamiaji
wa hivi karibuni kutoka
Laos
(1-2%),
Vietnam
,
Lebanoni
n.k.
Lugha rasmi
na ya kawaida ni
Kifaransa
.
Upande wa
dini
, wakazi walio wengi ni
Wakristo
wa
Kanisa Katoliki
(66.7%).
Tazama pia
Viungo vya nje
|
Makala hii kuhusu maeneo ya
Amerika Kusini
bado ni
mbegu
.
Je unajua kitu kuhusu
Guyani ya Kifaransa
kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|