Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Forbes
ni
gazeti
la
kibiashara
la
Marekani
ambalo huchapishwa mara
mbili
kwa
wiki
, huku likiangazia masuala ya
fedha
,
viwanda
,
uwekezaji
na
masoko
. Forbes pia humulika mambo yanayoendana na hayo, yakiwamo masuala ya
teknolojia
,
mawasiliano
,
sayansi
,
siasa
na
sheria
. Washindani wao katika biashara ya magazeti kitaifa ni pamoja na
Fortune
na
Bloomberg Businessweek
.
Gazeti hili hujulikana sana kwa kutoa
takwimu
,
orodha
na
madaraja
ya vitu/mambo mbalimbali kama vile takwimu ya Orodha ya
watu
tajiri
zaidi nchini Marekani (the
Forbes 400
) na madaraja ya
makampuni
makubwa zaidi
duniani
(the
Forbes Global 2000
). Orodha nyingine maarufu iliyowahi kufanywa na Forbes ni orodha ya
mabilionea
wakubwa zaidi duniani
The World's Billionaires
[1]
.
Kaulimbiu
ya gazeti la Forbes ni ("
The Capitalist Tool
") na
mhariri mkuu
(chief editor) wake ni
Steve Forbes
, na
mkurugenzi
(Chief executive officer) wake ni
Mike Perlis
.
Makao makuu
yake yapo katika
jiji
la
Jersey City
,
New Jersey
, lakini ilitangazwa mnamo
18 Julai
2014
kwamba
wanahisa
wakubwa wa gazeti hilo ni kutoka
Hong Kong
,
China
.
[2]
[3]