Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Brexit
(tamka Brek-sit) ni
kifupi
cha
British exit from the European Union
yaani mchakato wa
Ufalme wa Muungano
(
Great Britain
, "Uingereza") kuondoka katika
Umoja wa Ulaya
.
Tarehe 23 Juni 2016 kulikuwa na
kura ya maoni
katika Ufalme wa Muungano kuhusu swali la kubaki au kuondoka katika Umoja wa Ulaya ambako asilimia 51.9% walipigia kura hoja la kuondoka ilhali wengine walipendelea nchi kuendelea kama mwanachama wa Jumuiya ya Ulaya.
Kutokana na kura hii, serikali ya Ufalme wa Maungano ilitangaza nia yake ya kuondoka kwa kujulisha Umoja wa Ulaya rasmi kwenye tarehe 29 Machi 2017. Kufuatana na fungu 50 la
Mkataba kuhusu Umoja wa Ulaya
, baada ya tamko la nchi mwanachama kuwa inataka kundoka, kuna kipindi cha miaka miwili ambako mapatano kuhusu namna ya kuondoka yatajadiliwa, pamoja na mapatao kuhusu uhusiano wa nchi husika na umoja kwa miaka ya baadaye.
Kukwama kwa mapatano ya kuondoka
[
hariri
|
hariri chanzo
]
Ufalme wa Muungano ulitakiwa kuondoka kisheria baada ya miaka miwili tarehe 29 Machi 2019
[1]
. Serikali ya ya waziri mkuu
Theresa May
ilipatana na Umoja wa Ulaya kuhusu utaratibu wa kuondoka. Lakini tarehe 15 Januari 2019, 12 Machi na tena 29 Machi 2019 serikali ilishindwa kupata kibali cha bunge kwa mapatano yaliyoandaliwa.
[2]
Tatizo kuu lilikuwa hali ya mpaka baina ya
Jamhuri ya Eire
(Ireland)
na
Eire ya Kaskazini
(Northern Ireland)
. Hapo mapatano yalilenga kuepukana na "mpaka mgumu" baina pande mbili za kisiwa hiki lakini kwa mashariti ya Ufalme wa Muungano kubaki ndani ya eneo la ushuru la pamoja na Umoja wa Ulaya. Wapinzani waliogopa kuwa ama Ufalme wa Muungano ungepaswa kuendelea daima ndani ya utaratibu wa Umoja wa Ulaya au kutokea kwa mpaka baina ya Eire ya Kaskazini na sehemu nyingine za ufalme.
Baada ya kukosekana kwa wabunge wa kutosha wa kukubali pendekezo hili tarehe ya kuondoka ilibadilishwa baadaye kuwa 31 Oktoba 2019.
[3]
Muda wa nyongeza ulikusudiwa kuacha nafasi kwa mapatano ya utaratibu wa kuondoka. Bila mapatano ya aina hii Ufalme wa Muungano unabaki kama nchi yoyote nje ya Ulaya pamoja na haja ya kutimiza mashariti yote ya ushuru wakati wa kupokea au kutuma bidhaa Ulaya. Ilhali uchumi wa Uingereza uliwahi kukua kama sehemu ya Ulaya tangu 1973 bila kujali mipaka badiliko hili lilitazamiwa kuleta matatizo mazito. Bunge la Ufalme lilikataa mara kadhaa mfumo wa Brexit kali ("hard Brexit") bila kukubali mapatano yaliyoandaliwa na serikali ya May. Watetezi wa Brexit kali walionyesha matumaini kuwa nchi itafaulu kufanya mapatano mapya ya biashara na Marekani na nchi ya Asia.
Waziri mkuu May alijiuzulu na
Boris Johnson
alichukua nafasi yake. Johnson alitangaza kwamba Ufalme wa Muungano utaondoka katika Umoja wa Ulaya ama kwa mapatano mapya au pia bila mapatano.
|
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu
Brexit
kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|