Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Atanasi Bazzekuketta
(
1866
-
Nakivubo
27 Mei
1886
) ni
mfiadini
mmojawapo kati ya
Wakristo
22 wa
Kanisa Katoliki
wanaojulikana na kuheshimiwa duniani kote kama
Wafiadini wa Uganda
.
Hao walikuwa wahudumu wa
ikulu
ya
kabaka
wa
Buganda
Mwanga II
(
1884
-
1903
) ambao waliuawa kati ya tarehe 15 Novemba 1885 na tarehe
27 Januari
1887
kwa sababu ya kumwamini
Yesu Kristo
baada ya kuhubiriwa
Injili
na
Wamisionari wa Afrika
walioandaliwa na
kardinali
Charles Lavigerie
.
Hawa ndio wafiadini wa kwanza wa
Kusini kwa Sahara
kuheshimiwa na Kanisa Katoliki kama
watakatifu
.
Sikukuu
yao huadhimishwa tarehe
3 Juni
, lakini ya kwake mwenyewe tarehe
27 Mei
[1]
.
Siku hiyo, wakati wa kupelekwa kuuawa pamoja na wenzake, aliwaomba watesi wammalize haraka, nao wakampiga fimbo hadi kufa. Alikuwa
amebatizwa
tangu muda mfupi tu
[2]
.
|
Makala hii bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuiongezea habari
.
|