Wasandawe
ni
kabila
linaloishi hasa katika eneo la
wilaya
ya
Chemba
, mkoa wa
Dodoma
, katikati ya nchi ya
Tanzania
.
Wasandawe katika
wilaya ya Chemba
wanaishi hasa katika
tarafa
mbili, yaani
Farkwa
na
Kwamtoro
.
Wengi ni wafupi na wa
rangi
ya
weupe
/
njano
.
Wanawake
wana maumbo ya kuvutia na
wanaume
wana muonekano wa pekee.
Mpaka mwaka
2012
kabila hilo la pekee lilionekana katika vipimo kuwa na
viini nasaba
vya zamani kuliko makabila yote duniani
[1]
.
Kinasaba ndugu zao wa jirani ni hasa
Wakhoisan
wa
Kusini mwa Afrika
(
Botswana
,
Namibia
,
Afrika Kusini
na
Angola
. Wanajulikana kama "watu wa kwanza" na ndio wenyeji wakongwe zaidi kusini mwa Afrika. Wakaguzi na wageni wametazama kwa watu wa Bushmen kwa dalili za jinsi wanadamu walivyoweza kuishi katika
Zama za Mawe
), halafu
Waethiopia
.
Mwaka
2000
idadi ya Wasandawe ilikadiriwa kuwa 40,000
[2]
, na mwaka
2013
60,000, wengi wao wakiwa
Wakristo
, hasa
Wakatoliki
.
Lugha
yao ni
Kisandawe
, ya jamii ya
Kikhoisan
: ina
fonimu
nyingi kuliko lugha zote duniani, zikiwa ni pamoja na "click sounds". Inafikiriwa kuwa ya zamani kuliko zote, kwa kuwa inafanana bado na zile za wenzao Kusini mwa Afrika, ingawa walitengana miaka 40,000 hivi iliyopita. Inasemekana ni lugha tamu isiyochosha kusikiliza.
Miaka ya nyuma wengi wao walikuwa hawajasoma bali sasa wanasomesha vijana wao, hasa baada ya kuanzishwa
shule za kata
kama Farkwa Secondary, Kwamtoro Secondary, Makarongo Secondary, Gwandi Secondary, Kurio Secondary n.k.
Vilevile Wasandawe wengi wanajihusisha na
kilimo
japo bado wanaendelea na
uwindaji
, kwa kuwa
chakula
chao cha asili ni
nyama
.
- Bauer, Andreus. "Street of Caravans"
- Iliffe, John. "A Modern History of Tanganyika"
- "Mankind, the Illustrated Encyclopedia of" Pub. Marshall Cavendish
- Prince, Tom von.
Gegen Araber und Wahehe
|
Makala hii kuhusu utamaduni wa
Tanzania
bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu
Wasandawe
kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|