Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Wamarekani Weusi
ni watu wanaoishi nchini
Marekani
wakiwa na ma
babu
waliotoka
Afrika
.
Mara nyingi mababu hao walipelekwa Marekani kama
watumwa
katika
karne
zilizopita.
Jina
hili linaweza kutaja pia watu ambao
wazazi
wao au wenyewe walihamia Marekani hivi karibuni tu kutoka Afrika au kutoka nchi nyingine, hasa za
Karibi
na
Amerika Kusini
.
Watumwa walipelekwa Marekani kutoka Afrika kati ya miaka
1619
na
1807
hasa wakati usafirishaji wa watumwa kutoka Afrika ulipigwa
marufuku
.
Katika
utamaduni
wa Marekani kila mtu mwenye babu Mwafrika huhesabiwa kama "mtu mweusi" hata kama
urithi wake wa kinasaba
ni wa ki
chotara
na sehemu kubwa ni wa
Kizungu
.
Utafiti kwamba kwa wastani,
damu
yenye asili ya Afrika imechangia 78.1%, ile ya
Ulaya
18.5% na ya
Kiindio
3%.
Siku hizi Wamarekani weusi wengi huishi
mijini
lakini bado kuna maeneo yenye Wamarekani weusi wengi
mashambani
kusini mwa nchi.
Kwa jumla kuna watu 39,151,870 wanaohesibwa kama Waamerika weusi na hao ni asilimia 13.5 ya Wamarekani wote. Wengi wao ni
Wakristo
Waprotestanti
.
Mashuhuri kati ya Wamarekani weusi ni wanamuziki kama
Louis Armstrong
, wanasiasa kama
Martin Luther King, Jr.
au
Barack Obama
na waandishi kama
Toni Morrison
.