Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Shirika la kimataifa la kazi
(kwa
Kiingereza
:
International Labour Organization
;
kifupi
:
ILO
) ni wakala wa
Umoja wa Mataifa
wenye
mamlaka
ya kuendeleza
haki
za kijamii na kukuza
heshima
ya
kazi
kwa kuweka viwango vya kazi vya kimataifa (International labour standards).
[1]
ILO ni shirika maalum la kwanza la Umoja wa Mataifa. Lina
mataifa
washirika takribani 187: 186 kati ya mataifa washirika 193 wa Umoja wa Mataifa pamoja na
Cook islands
. Wawakilishi wa
serikali
, waajiri pamoja na waajiriwa hujumuika pamoja katika kujadili na kutengeneza viwango vya kazi.
Ofisi ya kazi ya kimataifa ni sekretarieti ya kudumu ya shirika la kimataifa la kazi (ILO). Ni zingatio katika shughuli za shirika la kimataifa la kazi ambazo inaziandaa chini ya uangalizi wa bodi ya utawala ambayo inaongozwa na
mkurugenzi
mkuu.
Shirika la kimataifa la kazi limeajiri maafisa 2,700 kutoka mataifa yote 150 na
makao makuu
yake yapo
Geneva
, pamoja na ofisi takribani 40 kote ulimwenguni. Baadhi ya maafisa, wapatao 900, wanafanya kazi katika kitengo cha mpango wa ushirikiano wa kiufundi na miradi.
Mnamo
mwaka
1969
,Shirika la kimataifa la kazi lilipokea
Tuzo ya Nobel ya Amani
(Nobel Peace Prize) kwa kuboresha undugu na amani kati ya mataifa, na kushawishi haki ya jamii kwa
wafanyakazi
na kutoa msaada wa kiufundi kwa mataifa yanayoendelea.
[2]
- ↑
"Mission and impact of the ILO"
.
ilo.org
.
- ↑
"The Nobel Peace Prize 1969"
.
Nobelprize.org
. Iliwekwa mnamo
5 Julai
2006
.
{{
cite web
}}
: CS1 maint: date auto-translated (
link
)
Wikimedia Commons ina media kuhusu: