Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Blimp ya kampuni ABC yatangaza matairi ya Goodyear
Blimp ya "Spirit of Dubai" yatangaza mradi wa Dubai "Palm Jumeirah"
Muundo wa Zeppelin yenye fremu imara
Zeppelin NT ya kisasa juu ya mji wa Frankfurt
Ndegeputo
(au
purutangi
) ni
chomboanga
kinachoelea kwa nguvu elezi ya
gesi
iliyoko ndani ya ganda lake. Chini ya chumba cha gesi inabeba behewa ya abiria na mizigo. Inasukumwa na injini za
parapela
.
Kimsingi kuna aina mbili za ndegeputo:
Ndegeputo isiyo na fremu ("Blimp")
[
hariri
|
hariri chanzo
]
Kimsingi aina hii ni fuko kubwa lenye gesi nyepesi (
heli
) ndani yake linalobeba behewa chini yake. Injini zafungwa kwenye behewa. Faida yao ni ya kwamba ni rahisi kuzisafirisha kwenye
nchi kavu
baada ya kuondoa gesi ndani yake. Fuko hukunjwa na haichukui nafasi kubwa. Bei si kubwa sana. Hasara ni ya kwamba haiwezekani kuongeza kukubwa juu ya kiwango fulani. Blimpu kubwa zinazopatikana hubeba hadi watu 10 au mzigo unaolingana.
Zapendwa sana kwa shughuli za matangazo ya kibiashara pia kwa safari za kitalii.
Kwa vyomboanga vikubwa zaidi ndegeputo zilipewa fremu ya ndani. Fremi hii yawezesha kufungwa kwa injini sehemu mbalimbali za chombo kinachoboresha uwezo wake wa kulengwa.
Kmapuni ya kwanza iliyoboresha muundo huo ilikuwa
Zeppelin
ya
Ujerumani
tangu mwaka
1900
. Usafiri wa mbali angani ulifanywa hasa kwa Zeppelin hadi maafa ya Lakehurst mwaka
1937
. Ndegeputo kubwa kabisa ilichomwa moto kwa sababu ilijazwa gesi ya
hidrojeni
ilishikwa na moto.
Ndegeputo za baadaye zilijazwa
heli
ambayo ni gesi nyepesi yenye uwezo mdogo wa nguvu elezi kuliko hidrojeni lakini haishiki moto.
Lakini usafiri wa abiria ulikwama baada ya maafa ya 1937 halafu ulipitiwa na maendeleo ya ndege.
Leo hii kampuni ya Zeppelin imeanza tena kujenga ndegeputo kwa mfumo ulioboreshwa wa "NT" ("neue Technologie/new technology" -
teknolojia mpya
) .
Huduma za kwanza za usafiri wa angani zilitekelezwa na ndegeputo. Tangu
vita kuu ya kwanza ya dunia
ndege ziliendelea zikaonekana ya kwamba zilikuwa usafiri wa haraka zaidi lakini hazikufika mbali bado. Ndege zilihitaji kushuka na kuongeza petroli kila baada ya masaa kadhaa lakini ndegeputo kubwa ziliweza kukaa hewani kwa siku mfululizo. Kabla ya
vita kuu ya pili ya dunia
ndegeputo za Zeppelin zilikuwa vyomboanga vya pekee vilivyosafirisha abiria mara kwa kati ya
Ulaya
na nchi za
Amerika
.
Maendeleo ya ndege wakati wa vita kuu ya pili ya dunia na baadaye imeondoa ndegeputo katika usafiri wa kawaida. Ndege hubeba abiria na mizigo haraka zaidi, hubeba mizigo mikubwa zaidi tena katika kila
hali ya hewa
wakati ndegeputo zina matatizo kama upepo ni mkali mno au halijoto yapanda mno inayosababisha gesi ndani ya ganda kuenea sana.
Siku hizi ndegeputo zatumiwa hasa kwa shughuli tatu:
- fuko la gesi latumiwa kwa
matangazo ya kibiashara
. Ni hasa blimp ndogo zinazokodishwa kuonyesha matangazo haya juu ya miji mikubwa au penye mikutano ya watu wengi.
- kwa
safari za kitalii
kwa muda mfupi ndegeputo ina faida ya kutembea polepole kwenye kimo kidogo hali inayowezesha abiria kutazama vizuro yote yaliyopo chini yao.
- kwa
utafiti wa kisayansi
na
shughuli za usimamizi
; uwezo wa kulea polepole kwa kimo kidogo tena kwa muda mrefu wawezesha vipimo vya kisayansi kufanyiwa kwa makini kushinda vipimo kwa njia za ndege.
- Faida hii yatumiwa pia kibiashara. Zeppelin NT mpya imekodiwa na kampuni
De Beer
ya
Afrika Kusini
tangu
2005
kwa vipimo vya kutafuta
almasi
katika
Botswana
na inasemekana kwa matokeo bora kushinda vipimo vya awali kwa ndege au helikopta.
- Ndegeputo zatumiwa kwa usimamizi wa mikutano mikubwa kwa mfano
michezo ya Olimpiki
ya
Athens
ya
2004
au mkutano wa vijana wa dunia wa kanisa katoliki huko
Koln
mwaka
2006
.