Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mchezo wa ngumi
ni aina ya
michezo ya mapigano
ambapo ma
bondia
wawili wanapigana kwa kutumia
ngumi
pekee kwa kufuata kanuni za mchezo. Wote wawili huvaa
glavu
nene kwa shabaha ya kupunguza hasara za kiafya.
Mashindano yasimamiwa na
refa
, kwa kawaida mbele ya watazamaji na kutekelezwa ndani ya mzingo maalumu.
Mashindano yamegawiwa kwa vipindi vinavyodumu
dakika
1 - 3. Shabaha ni ama kumpiga mshindani hadi asiweze kuendelea tena au kufikisha mapigo mengi
kichwani
na
tumboni
yatakayohesabiwa na refa na kuamulisha ushindi.
Historia
Watu waliwahi kupigana kwa kutumia ngumi kwa kufuata kanuni fulani tangu
milenia
nyingi.
Mchezo wa ngumi jinsi ulivyoenea leo kote
duniani
ulianza
Uingereza
katika
karne ya 19
.