Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Maurice Michael Otunga
(Januari
1923
-
6 Septemba
2003
) alikuwa
askofu
wa
kanisa katoliki
na
kardinali
wa kwanza nchini
Kenya
.
Otunga alizaliwa mwaka 1923 kwenye kijiji cha Chebukwa katika wilaya ya
Bungoma
. Babake alikuwa chifu wa koo la Bakhone katika kabila
Wabukusu
mwenye wake 40.
Maurice alibatizwa kwa umri wa miaka 12 akamaliza masomo yake ya shule Mangu High School. Baadaye akajiunga na seminari ya
Kakamega
akaendelea masomo ya upadre kwenye semianri ya Gaba (
Kampala
-
Uganda
). Masomio ya juu akafuata huko
Roma
kwenye chuo kikuu cha Papa alipopadrishwa mwaka 1950 pamoja na kupokea cheo cha daktari.
Baada ya kurudi Kenya akawa mwalimu kwenye seminari ya
Kisumu
hadi 1956 alipoteuliwa kuwa askofu msaidizi wa Kisumu.
1960 alikabidhiwa dayosisi mpya ya Kisii kama askofu wake wa kwanza. 1969 akawa msaidizi wa askofu kuu wa Nairobi na 1971 alikuwa askofu mkuu wa kwanza Mwafrika.
Tar. 5 Machi
1973
Papa Paulo VI
akampa cheo cha kardinali.
Otunga akajiuzulu 1997 alipofikia umri wa miaka 75 akachagua nyumba ya wazee maskini kama makao yake ya uzeeni.
Kardinali Maurice Michael Otunga aliaga dunia 6 Septemba 2003 akiwa na umri wa miaka 80.
Mwaka 2005 kulitokea fitina juu ya kaburi lake kati ya kanisa katoliki na jumuiya ya Wabukusu. Askofu Mkuu
Mwana a'Nzeki
alimua kuhamisha maiti ya kardinali kutoka makaburi ya mjini kwenda Resurrection Gardens na kumzika katika kanisa dogo huko wakati kanisa la Kenya lafuatilia shughuli za kumtangaza marehemu kuwa mwenye heri. Wasemaji wa Wabukusu walipinga mipango hii kwa hofu ya kwamba tendo litaleta balaa juu ya kabila.