Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Maria Teresa Goretti
(
Corinaldo
,
Ancona
,
Italia
,
16 Oktoba
1890
-
Nettuno
,
Lazio
,
6 Julai
1902
) alikuwa
bikira
Mkristo
ambaye, baada ya kupitia
utoto
katika
ufukara
akimsaidia
mama
yake
mjane
katika shughuli za
nyumbani
na kudumu katika
sala
, alikataa mfululizo
kuzini
na
jirani
yake
Alessandro Serenelli
, mpaka huyo akamchoma mara 14 mfululizo kwa
kifaa
cha
chuma
[1]
.
Akizidi kuchomwa, Maria alisisitiza msimamo wake: "Usifanye, ni
dhambi
!"
Kabla hajafa
hospitalini
, Maria alimsamehe muuaji wake kwa kumtakia awe naye
mbinguni
.
Baada ya miaka mitatu
gerezani
, Alessandro
aliongoka
na alipotoka alikwenda kuomba
msamaha
wa
mama
wa Maria, akakubaliwa kwa hoja kwamba, "Mwanangu amekusamehe wakati wa kufa, nami siwezi kufanya tofauti". Kesho yake walipokea
ekaristi
pamoja.
Halafu akaishi
utawani
kwa
Wakapuchini
wa
Macerata
hadi alipofariki mwaka
1970
.
Alitangazwa na
Papa Pius XII
kuwa
mwenye heri
tarehe
27 Aprili
1947
na kuwa
mtakatifu
tarehe
24 Juni
1950
, wakihudhuria mama yake na muuaji vilevile.
Sikukuu
yake inaadhimishwa tarehe ya
kifodini
chake,
6 Julai
ya kila mwaka
[2]
.
- Beatificationis seu declarationis martyrii Mariae Goretti
, Roma, 1938-1939 (nyaraka za kesi ya kumtangaza mwenye heri).
- Compendium vitae virtutum ac miracolorum Beatae Mariae Theresiae Goretti
, Typis Polyglottis Vaticani, 1950 (nyaraka za kesi ya kumtangaza mtakatifu).
- A proposito di Maria Goretti: santita e canonizzazioni: atti della Commissione di studio istituita dalla Congregazione per le cause dei santi il 5 febbraio 1985
, Citta del Vaticano,
Libreria Editrice Vaticana
, 1986.
- Giovanni Alberti,
Maria Goretti
,
Citta Nuova Editrice
, 1980.
ISBN 88-8386-150-7
.
- Giordano Bruno Guerri
,
Povera santa, povero assassino. La vera storia di Maria Goretti
,
Mondadori
, Milano,
1985
- toleo jipya lililorekebishwa na kuongezewa
Bompiani
, Milano,
2008
.
|
Makala hii bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuiongezea habari
.
|