Mapito ya kaskazini-magharibi
ni njia ya
bahari
inayoruhusu kupita kutoka
Atlantiki
kufika
Pasifiki
(na kinyume) upande wa
kaskazini
wa
Amerika
. Njia hiyo inapita katika
Bahari Aktiki
na kwa sababu ya wingi wa
barafu
katika sehemu hizo za kaskazini, kwa kawaida hakupitiki na
meli
. Lakini siku hizi barafu inapungua na kuruhusu mipango ya kuunda njia mpya za
mawasiliano
,
biashara
na kuendeleza
uchumi
wa nchi zinazopakana na Aktiki.
Historia za kutafuta mapito ya kaskazini-magharibi
[
hariri
|
hariri chanzo
]
Hamu ya mataifa ya Ulaya kupata njia ya bahari kufika Asia
[
hariri
|
hariri chanzo
]
Tangu
karne za kati
mataifa
ya
Ulaya Magharibi
walitafuta njia ya kufikia
Uhindi
na
China
, nchi ambazo
bidhaa
zao zilifika tu
Ulaya
kwa
bei
ghali sana kupitia kwa
wafanyabiashara
Waislamu
wa
Asia ya Magharibi
.
Wareno
walitangulia kuvuka
Afrika
na kufika Uhindi na
Asia Kusini Mashariki
; kwa nia ya kuepukana na ugomvi kati ya mataifa mawili jirani,
wafalme
wao na wa
Hispania
walipatana
mwaka
1494
katika
Mkataba wa Tordesillas
kwa msaada wa
Papa
kugawa kati yao maeneo mapya ya
Dunia
yatakayovumbuliwa;
Wahispania
waliahidiwa maeneo upande wa
magharibi
wa mstari uliofuata
longitudo
ya 46° 37′. Waliendelea kutafuta njia ya kuzunguka
Amerika
ili waweze kuendelea hadi China na Uhindi.
Mwaka
1520
nahodha
Magellan
alivuka
pembe
ya
kusini
ya Amerika akaingia katika Pasifiki na kuwezesha wasafiri wenzake kumaliza mzunguko wa Dunia.
Kutafuta njia mbadala upanda wa kaskazini-magharibi
[
hariri
|
hariri chanzo
]
Ilikuwa dhahiri kwamba njia kutoka Ulaya hadi China ingekuwa karibu na nafuu kabisa kama njia ya kupita upande wa kaskazini ingepatikana. Mapito ya kaskazini-magharibi yanafupisha
safari
kati ya Ulaya na Asia Mashariki kiasi cha
kilomita
4,000.
Hii ilileta uhamasisho mkubwa kwa mataifa ya Ulaya Magharibi kutafuta mapito hayo ya kasakazini-magharibi.
Mabaharia
na
wapelelezi
Wahispania,
Wafaransa
,
Waitalia
,
Wadenmark
,
Waingereza
na wengine walijaribu kukuta njia hiyo. Waliingia katika
mito
mikubwa na
hori
zilizoweza kufikiwa kutoka
pwani
ya Atlantiki lakini njia hizo hazikufika hadi Pasifiki. Wakaendelea kuelekea kaskazini wakiingia kati ya visiwa vya Aktiki lakini mara kwa mara walisimamishwa na
ukuta
wa barafu.
Ugumu wa mazingira asilia kwenye Aktiki
[
hariri
|
hariri chanzo
]
Hali halisi hakuna njia rahisi kwa meli na
jahazi
za zamani kwa sababu ya wingi wa barafu; hata katika miezi ambapo
halijoto
ya
hewa
inapanda juu na barafu ya bahari inaanza kuvunjika, vipande vikubwa vya barafu vinaelea kwenye maji yanayoweza kuzamisha hata meli kubwa.
Roald Amundsen
alikuwa
mtu
wa kwanza aliyefaulu kusafiri kwenye mapito ya kaskazini akilazimishwa kupumzika njia mara mbili na kusubiri hadi
baridi
kali ilipokwisha na barafu ilipoyeyuka tena.
Meli ya kwanza iliyoweza kupita bila kupumzika ilikuwa SS
Manhattan
katika
Septemba
1969
katika
muda
wa
wiki
nne
. Meli hiyo iliwahi kuimarishwa kwa
feleji
nyingi ili kuiwezesha kusukuma pande kubwa za barafu zinazoelea majini na kuvunja barafu. Laini meli ilihitaji matengezo mengi baada ya safari.
Mabadiliko ya tabianchi na kufunguliwa kwa njia ya kaskazini
[
hariri
|
hariri chanzo
]
Ni tangu
kupanda kwa halijoto duniani
katika miongo iliyopita kwamba barafu katika eneo la Aktiki imeanza kupungua. Tangu mwaka
2008
meli chache zimeanza kubeba mizigo kupitia njia hii wakitumia wiki chache ambapo barafu imevunjika kwa uhakika.
Baada ya mwaka
2010
safari hizo ziliongezeka.
Kadiri barafu ya Aktiki inavyopungua kipindi cha mwaka ambapo uwezekano wa kupita upo unaongezeka.
Tayari
viumbehai
vya kwanza kutoka Pasifiki ya kaskazini vimeanza kuingia Atlantiki, mfano
planktoni
ya Pasifiki na pia
spishi
za
nyangumi
ambazo hazikuwepo upande huu.
|
Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni
mbegu
.
Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuiongezea habari
.
Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.
|