Mapinduzi ya Ufaransa
(kwa
Kifaransa
:
Revolution francaise
) ni
jina
linalojumlisha matukio muhimu ya
siasa
kwa kipindi cha miaka 10, tangu
1789
hadi
1799
, yaliyobadilisha uso wa
Ufaransa
na
utamaduni
wa
Ulaya
kwa jumla, kiasi cha kuhesabiwa kati ya matukio makuu ya
historia
yote.
[1]
[2]
[3]
Kupitia
vita
mbalimbali vilivyofuata katika sehemu mbalimbali za
dunia
,
[4]
athira
zake zilieneza kote
duniani
fikra
za
haki za binadamu
,
uhuru
na
maendeleo
zilizotetewa na
Falsafa ya Mwangaza
.
[5]
Dhana
ya kuwa
mamlaka
juu ya
dola
ni
haki
ya
raia
wote, si ya
wafalme
wala
watawala
wengine,
[6]
imeenea polepole pande zote za
dunia
.
[7]
Pamoja na hayo,
mapinduzi
na matukio yaliyofuatwa yalisambaza mtazamo hasi kuhusu
dini
, huhusan
Ukristo
na
Kanisa Katoliki
, kwa kudai
akili
ishike nafasi ya
imani
pia.
Mwaka 1789
mfalme
Louis XVI
alilazimishwa kuitisha
bunge
la
taifa
kwa mara ya kwanza baada ya miaka 170. Sababu yake ilikuwa kwa kiasi kikubwa cha
madeni
ya
serikali
yaliyosababishwa na matumizi makubwa ya mfalme pamoja na
gharama
za
vita vya uhuru
vya
Marekani
vilivyosaidiwa na Ufaransa dhidi ya
Uingereza
.
[8]
Tangu
Louis XIV
(
1643
?
1715
) wafalme walitawala Ufaransa bila bunge, lakini kisheria mfalme hakuwa na
madaraka
ya kuongeza
kodi
bila
idhini
ya bunge, na Louis XVII hakuwa tena na nguvu ya kutosha kupuuzia utaratibu huo.
Bunge la Ufaransa lilikuwa na wawakilishi wa
matabaka
matatu: koo za
makabaila
, wawakilishi wa
Kanisa Katoliki
na wawakilishi wa tabaka la tatu yaani raia waliolipa kiasi fulani cha kodi.
Maskini
na
wanawake
hawakuwa na wawakilishi.
Wawakilishi wengi wa tabaka la tatu walidai kupewa nafasi kubwa zaidi kuliko matabaka mengine. Baada ya matatizo ya kutoelewana, kwenye tarehe
17 Juni
1789
wawakilishi wa tabaka la tatu walijitangaza kuwa bunge la taifa hata bila ya wawakilishi wa waungwana waliotetea haki zao za kale.
Kutokana na vurugu za kisiasa na
mfumuko wa bei
za
chakula
, wananchi wa
Paris
waliasi, wakashambulia
gereza
la
Bastille
tarehe
14 Julai
na kulibomoa. Tarehe hiyo hadi leo ni sikukuu ya mapinduzi nchini Ufaransa. Mfalme aliyedhoofika hakutaka kukandamiza
uasi
huo na bunge la taifa liliendelea kubadilisha
sheria
kwa kufuta haki za pekee za waungwana.
Mashambani
wakulima
walianza kuasi na kukataa ulipaji kodi katika
mikoa
mbalimbali.
Mfalme alipoona ya kwamba madaraka yake yanapungua zaidi na zaidi alijaribu kuondoka lakini alikamatwa na kurudishwa kama mfungwa mwaka
1791
.
Mwelekeo mkali kati ya wabunge ulipata
ushindi
na mwaka
1792
Ufaransa ulitangazwa kuwa
jamhuri
. Mfalme alishtakiwa kuwa
msaliti
wa taifa akapewa
hukumu ya kifo
na kukatwa
kichwa
pamoja na
mke
wake tarehe
21 Januari
1793
.
Wafalme wa nchi jirani waliamua kushambulia Ufaransa na kulipiza
kisasi
kwa
kifo
cha mfalme. Katika joto la
vita
watu wa vikundi vikali vilipata
kipaumbele
wakaanzisha kipindi cha
udikteta
chini ya kamati ya bunge lililoongozwa na
Robespierre
. Watu wengi (16,000-40,000) walishtakiwa kuwa wasaliti wakauawa
[9]
hadi
upinzani
ndani ya bunge ulipofaulu kuwakataa viongozi wakali na kuwaua.
Kipindi kilichofuata kilikuwa na serikali zilizochaguliwa na bunge. Zililenga kurudisha utaratibu nchini na kutetea taifa katika vita vilivyoendelea hasa dhidi ya
Uingereza
na
Austria
.
Katika vita hivyo
jenerali
Napoleon Bonaparte
alikuwa kiongozi aliyeweza kushinda Austria akawa
shujaa
wa taifa. Mwaka
1799
kwa tishio la kijeshi alilazimisha bunge kubadilisha
katiba
akaingia serikalini na kuwa
mtawala
pekee kwa
kibali
cha bunge lisilokuwa na njia nyingine isipokuwa kumkubali.
Tangu hapo Napoleon alitawala kwa
cheo
cha "
konsuli
wa kwanza". Baada ya mabadiliko mengine ya katiba alichukua cheo cha
Kaisari
wa Ufaransa mwaka
1804
.
Kabla ya mapinduzi Ufaransa ulitawaliwa na wafalme. Mfalme
Louis XIV
aliwahi kuunganisha mamlaka yote ya dola mikononi mwake akifaulu kukandamiza upinzani wote wa
waungwana
na
malodi
. Utawala huo wenye madaraka yote uliendelea chini ya waaandamizi wake. Kila azimio lilitegemea mapenzi ya mfalme bila njia yoyote ya upinzani.
Ufaransa haukuwa na bunge la kudumu; palikuwa na mabunge ya kimkoa ambako wawakilishi wa waungwana na ma
kasisi
wakuu wa Kanisa Katoliki (iliyokuwa
dini pekee halali kisheria
) walikutana, wakati mwingine pamoja na wawakilishi kadhaa wa
tabaka la tatu
lililojumlisha watu wengine wote wenye
mali
. Bunge la taifa lililokuwa na madaraka ya kuamua juu ya sheria za kodi hasa liliwahi kualikwa mara kadhaa na wafalme lakini tangu Louis XIV halikukutana tena.
Mwaka 1789 utawala huo ulishikwa na mchafuko. Wafalme waliwahi kutumia
pesa
vibaya na nchi ilikuwa na madeni makubwa. Madeni hayo yalisababishwa na vita, matumizi makubwa kwa ma
afisa
wa serikali na
gharama
za
familia
ya kifalme, kwa mfano
ujenzi
wa majumba ya kifalme na
sherehe
za mfalme.
Katika
jamii
ya Ufaransa vikundi viwili vilikuwa na haki nyingi, yaani familia za waungwana na makasisi wa Kanisa Katoliki. Hao hawakulipa kodi ingawa walikuwa na mashamba makubwa yaliyolimwa na wakulima waliopaswa kuwalipia mchango wa mavuno. Kodi zote za nchi zililipwa na wakulima au
wafanyabiashara
wa mjini.
Mwaka
1788
ulikuwa na mavuno mabaya na wakulima wengi hawakujua jinsi ya kulipa kodi zao.
Ghala
za waungwana na za ma
kanisa
zilijaa kutokana na mavuno ya miaka ya nyuma, lakini kwa jumla
bei
ya
nafaka
ilipanda pamoja na bei ya
mkate
uliokuwa chakula kikuu cha Wafaransa.
Viongozi wa serikali chini ya mfalme waliona
haja
ya mabadiliko lakini matabaka tawala ya waungwana na viongozi wa Kanisa hawakuwa tayari kukubali mabadiliko yoyote.
Mnamo Februari 1789 serikali ilialika mkutano wa wawakilishi wa waungwana na makasisi wakuu ikatafuta kibali chao kwa sheria mpya, eti hata waungwana walipe kodi. Mkutano ulikataa ukidai hauna madaraka ya kubadilisha sheria za kale, lakini ilikuwa wazi kwamba hiyo ilikuwa
lugha
tu ya kuepukana na kodi.
Hivyo serikali ilimshauri mfalme kualika bunge la kitaifa la matabaka yote matatu kwa mara ya kwanza tangu mwaka
1614
. Zamani bunge hilo lilikuwa na idadi sawa ya wawakilishi kwa kila tabaka yaani 300-300-300 kwa waungwana, makasisi na tabaka la tatu. Tena kila tabaka lilikuwa na
kura
moja tu, kwa hiyo kila azimio lilihitaji kura zote tatu au kura mbili dhidi ya moja.
Kabla ya mkutano huo wawakilishi wa tabaka la tatu walidai kuongezeka kwa kura zao wakieleza ya kwamba hadi sasa tabaka lao lililipa kodi zote na kuwakilisha zaidi ya
asilimia
90 za wananchi. Mfalme alihangaika akakubali tabaka la tatu liwe na wawakilishi 600, isipokuwa alikaa
kimya
juu ya suala la kura.
Kujitenga kwa tabaka la tatu kuwa bunge la taifa
[
hariri
|
hariri chanzo
]
Bunge lilikaa
wiki
kadhaa bila ya makubaliano juu ya namna ya kupiga kura. Baada ya
mwezi
mmoja sehemu ya ma
padri
walijiunga na wawakilishi wa tabaka la tatu kutetea azimio lililopelekwa na kasisi Abbe Siyes: tabaka la tatu likajitangaza kuwa linawakilisha asilimia 96 za wananchi likajiita "bunge la taifa". Wawakilishi wa waungwana na makasisi wengine walialikwa kujiunga nao kwenye msingi wa kura moja kwa kila mbunge.
Makasisi wengi na waungwana wachache walifuata
wito
huo, lakini kundi kubwa la waungwana walikataa wakadai mfalme aingilie kati. Mfalme Louis XVI alitangaza mkutano mpya chini ya utaratibu wa kale akafunga
ukumbi
wa mkutano hadi siku hiyo.
Wawakilishi wa bunge la taifa waliamua kukutana mahali penginepo wakaahidiana kutoachana hadi
katiba
ya taifa itakapokuwa tayari. Mfalme aliamuru waondoke lakini
mwenyekiti
wao alikataa. Mfalme aliandaa vikosi vya
jeshi
lakini sehemu za waungwana walimwomba asitumie
silaha
. Mwishowe mfalme alikata tamaa akaamuru matabaka yote yakae pamoja katika bunge la taifa.
- ↑
Linda S. Frey and Marsha L. Frey,
The French Revolution
(2004), Foreword.
- ↑
R.R. Palmer and Joel Colton,
A History of the Modern World
(5th ed. 1978), p. 341
- ↑
Ferenc Feher,
The French Revolution and the Birth of Modernity
, (1990) pp. 117-30
- ↑
Bell, David Avrom (2007).
The First Total War: Napoleon's Europe and the birth of warfare as we know it
. New York: Houghton Mifflin Harcourt. uk.
51
.
ISBN
0-618-34965-0
.
- ↑
Suzanne Desan et al. eds.
The French Revolution in Global Perspective
(2013) , pp. 3, 8, 10
- ↑
Livesey, James.
Making Democracy in the French Revolution
p. 19
The Revolution created and elaborated...the ideal of democracy, which forms the creative tension with the notion of sovereignty that informs the functioning of modern democratic liberal states. This was the truly original contribution of the Revolution to modern political culture.
- ↑
Palmer, R.R. & Colton, Joel
A History of the Modern World
p. 361
- ↑
Tombs, Robert and Isabelle.
That Sweet Enemy: The French and the British from the Sun King to the Present
. Random House (2007)
ISBN 978-1-4000-4024-7
. Page 179.
- ↑
Matusitz, Jonathan
Symbolism in Terrorism: Motivation, Communication, and Behavior
, p. 19
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
- Museum of the French Revolution
(French)
- Primary source documents
Archived
10 Aprili 2008 at the
Wayback Machine
. from The Internet Modern History Sourcebook.
- Liberty, Equality, Fraternity: Exploring the French Revolution
, a collaborative site by the Center for History and New Media (George Mason University) and the American Social History Project (City University of New York).
- Vancea, S.
The Cahiers de Doleances of 1789
, Clio History Journal, 2008.
- French Revolution Digital Archive
a collaboration of the Stanford University Libraries and the Bibliotheque nationale de France, containing 12000 digitised images
- The guillotined of the French Revolution
factsheets of all the sentenced to death of the French Revolution
- Jean-Baptiste Lingaud papers
Archived
2015-04-23 at
Archive.today
, Kislak Center for Special Collections, Rare Books and Manuscripts, University of Pennsylvania. Includes a vast number of name lists and secret surveillance records as well as arrest warrants for aristocrats and their sympathisers. Most notable in this part of the collection are letters and documents from the Revolutionary Committee and the Surveillance Committee.
- French Revolution Pamphlets
, Division of Special Collections, University of Alabama Libraries. Over 300 digitised pamphlets, from writers including Robespierre, St. Juste, Desmoulins, and Danton.
- "The French Revolution's Legacy"
BBC Radio 4 discussion with Stefan Collini, Anne Janowitz and Andrew Roberts (
In Our Time
, 14 June 2001)
- The Musee de Veygoux
- a museum in
Auvergne
dedicated to the French Revolution and
Desaix
- The declaration of the Rights of Man and of the Citizen
Archived
6 Juni 2013 at the
Wayback Machine
.
|
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu
Mapinduzi ya Ufaransa
kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|