Justino de Jacobis
(
San Fele
,
Potenza
,
Italia
,
9 Oktoba
1800
-
Eidale
,
Massawa
,
31 Julai
1860
) alikuwa
mtawa
wa
Shirika la Misheni
(
Wavinsenti
), halafu
askofu
na
mmisionari
nchini
Ethiopia
na
Eritrea
.
Anaheshimiwa na
Kanisa Katoliki
kama
mtakatifu
tangu tarehe
26 Oktoba
1975
. Hata
Wakristo
wengine na
Waislamu
wanatembelea
kaburi
lake kwa
heshima
.
[1]
Sikukuu
yake ni
tarehe
31 Julai
[2]
[3]
.
Akiwa
mtoto
wa saba wa Giovanni Battista de Jacobis na wa Maria Giuseppina Muccia, tarehe
17 Oktoba
1818
alijiunga na
utawa
huko
Napoli
akaweka
nadhiri
miaka miwili kamili baadaye.
Ingawa kwa
unyenyekevu
wake mkubwa alitaka kukataa, alipata
upadrisho
huko
Brindisi
tarehe
12 Juni
1824
.
Kisha kufanya
uchungaji
huko
Oria
na
Monopoli
, alifanywa mkuu wa kanda katika shirika lake kwanza
Lecce
halafu Napoli. Huko alijitosa kuhudumia waliopatwa na
kipindupindu
mwaka
1836
.
Akiwa huko alielezwa na
Kardinali
Franzoni juu ya haja ya
umisionari
nchini Ethiopia.
Mwaka
1839
alichaguliwa kuwa
mkuu wa kitume
nchini huko ili aanzishe
misheni
katoliki
.
Kwa
upole
na wingi wa
upendo
wake, Justino alijitahidi kujifunza vizuri
lugha
za nchi, kuishi pamoja na wenyeji, akifuata
utamaduni
wao na mifano ya
wamonaki
wao.
Vilevile katika
uinjilishaji
alitumia
mapokeo
na
liturujia ya Ethiopia
, akiweka
msingi
wa
Kanisa Katoliki la Waethiopia
na wa
Kanisa Katoliki la Waeritrea
.
Baada ya kufanya
kazi
hiyo kwa mafanikio makubwa miaka minane, mwaka
1847
aliteuliwa kuwa askofu wa
Nilopolis
na
makamu wa Papa
kwa
Uhabeshi
, ila alikataa
uaskofu
hadi alipolazimika mwaka
1849
.
Ingawa alipaswa kuvumilia
njaa
na
kiu
na kupata mapingamizi mengi hasa kutoka kwa
Abuna Salama II
,
askofu mkuu
wa
Kanisa la Kiorthodoksi la Ethiopia
(kufungwa, kufukuzwa n.k.), alifaulu kuanzisha misheni na
shule
nyingi hasa kwa lengo la kuandaa mapadri wenyeji
[4]
.
Hatimaye askofu mkuu huyo alikiri kwamba hakuna mtu aliyewahi kushika vizuri maagizo na mashauri ya
Injili
kuliko Justino.
Kati ya watu 12,000 hivi aliowaongoa, mmojawapo ni
mwenyeheri
Ghebre Mikaeli
.
Kesi
ya kumtangaza
mwenye heri
ilianza tarehe
13 Julai
1904
, ikamalizika tarehe
25 Julai
1939
chini ya
Papa Pius XII
.
Alitangazwa na
Papa Paulo VI
kuwa mtakatifu tarehe
26 Oktoba
1975
, akiwa wa kwanza kati ya wamisionari wa
Afrika
kusini kwa Sahara
.
- ↑
Tom Killion,
Historical Dictionary of Eritrea
, The Scarecrow Press, 1998,
ISBN 0810834375
- ↑
Martyrologium Romanum
- ↑
https://catholicsaints.info/saint-giustino-de-jacobis/
- ↑
https://www.santiebeati.it/dettaglio/33850
- Mkusanyo wa maandishi yake - Giuseppe Guerra - Ed. Vincenziani (kwa
Kiitalia
).
- Devin, A., (Traduzione inglese di Lady Elizabeth Herbert of Lea),
Abyssinia and its Apostle
, Burns and Oates, London, 1867
- Antonio Furioli,
L'eucaristia, epifania di dialogo e di comunione. Sua esemplarita in San Giustino de Jacobis
in
Rivista di ascetica e mistica
, 75 (aprile-giugno 2006) 2, 213-228.
- Antonio Furioli,
Il frutto piu prezioso dell'apostolato di San Giustino de Jacobis. Il Beato Gabra Mik?’?l (1791-1855), martire per la fede in Abissinia
in
Rivista di ascetica e mistica
, 75 (luglio-settembre 2006) 3, 385-403.
- Antonio Furioli,
Vangelo e testimonianza. L'esperienza di San Giustino de Jacobis in Abissinia (1839-1860)
, Milano, San Paolo, 2008.
|
Makala hii bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuiongezea habari
.
|