Julius von Soden
(
5 Februari
1846
-
2 Februari
1921
) alikuwa
mwanasiasa
wa
Ujerumani
aliyetawala
makoloni
mawili ya nchi hiyo
barani
Afrika
:
Kamerun
na
Afrika ya Mashariki ya Kijerumani
. Baadaye alikuwa
waziri
kwenye
serikali
ya
Ufalme wa Wurttemberg
katika Ujerumani kusini-magharibi.
Julius alizaliwa katika kambi la
jeshi
huko
Ludwigsburg
kusini-magharibi mwa Ujerumani.
Baba
yake alikuwa
luteni kanali
kwenye jeshi la Ufalme wa Wurttemberg.
Familia
walikuwa
Wakristo
wa
Kanisa la Kiinjili la Kilutheri
.
Mnamo mwaka wa
1849
familia
ilihamia
Stuttgart
. Wazazi wake walifariki mapema.
Mama
yake Marie von Neurath aliaga dunia tarehe
28 Machi
1849
, na baba yake Julius tarehe
13 Aprili
1854
. Soden na dada zake watatu wakubwa walilelewa na
bibi
Charlotte von Neurath,
mjane
wa
Waziri
wa
Sheria
wa Wurttemberg.
Soden alianza
shule
Korntal
, kisha akaenda
sekondari
huko
Stuttgart
. Mwalimu wake wa kwanza Julius Klaiber na walimu kwenye shule ya sekondari walimlea kwa upendo kwa elimu ya tamaduni za
Ugiriki
na
Roma ya Kale
. Katika
maisha
yake yote, Soden alipenda kusoma vitabu vya
waandishi
wa kale, hasa
Homer
na
Dante
. Mtazamo wake wa ulimwengu ulikuwa ukiathiriwa na mtheolojia
David Strauss
na mwanafalsafa
Emmanuel Kant
.
Baada ya kuhitimu shule mwaka wa
1864
, Soden alianza kujifunza sheria katika
Chuo Kikuu cha Tubingen
, lakini baadaye alihamia
Gottingen
.
Wakati wa
Vita ya Austria na Prussia
ya
1866
alijikuta kwenye matata maana Julius alipenda siasa ya waziri mkuu wa
Prussia
,
Otto von Bismarck
, wakati familia yake ilipenda
Austria
. Alibaki Gottingen kwa maelezo kwamba haikuwa rahisi kusafiri wakati wa
vita
, akarudi Tubingen kwa ajili ya
mitihani
yake mwaka
1869
.
Baada ya mtihani wa chuo alianza kazi ya sheria huko
Heilbronn
. Ilipofika
Vita ya Ufaransa dhidi ya Ujerumani ya 1870
Soden alijitolea akihudumu katika wapandafarasi wa Wurttemberg. Wakati wa
amani
alirudi kwenye kazi yake ya sheria hadi kumaliza mtihani wa pili katika mfumo wa Ujerumani mwishoni mwa
1871
.
Tokeo la ushindi juu ya Ufaransa lilikuwa umoja wa Ujerumani na kuundwa kwa
Dola la Ujerumani
. Dola jipya lilianza kutuma mabalozi kwenye nchi za kigeni. Soden alitumia nafasi hiyo akapata ajira kama mwanadiplomasia
Bukarest
mnamo 1871. Baada ya nusu mwaka alihamishwa
Algiers
aliposimamia ubalozi mdogo ulioanzishwa huko (1872).
1876 alihamishwa tena kwenda
Kanton (leo:Guangzhou)
na
Hong Kong
, 1879 alikwenda
Havana
. Uhamisho kwenda
Lima
(Peru) ulifuata 1881/82 kama makamu wa balozi na mwanzo wa 1884 alitumwa
Sankt Petersburg
.
[1]
Katika kazi yake alijifunza kwamba uendelezaji wa mawasiliano ya biashara ulipaswa kufanywa na wafanyabiashara, sio na wanadiplomasia.
Mwaka 1884 Ujerumani ilianzisha
koloni
yake ya kwanza huko Afrika ya Magharibi. Mnamo Julai 1884 Soden aliteuliwa kuwa kamishna mkuu wa
koloni ya Kijerumani ya Togo
. Mwaka uliofuata alipewa pia kazi ya kuwa gavana wa kwanza wa
Kamerun.
Kabla ya kusafiri kwa meli, von Soden alishauriwa na mmisionari
Friedrich Fabri
na makampuni yaliyofanya biashara
Afrika Magharibi.
Baada ya kuondoka kwa
chansela Bismarck
Soden alipenda kustaafu lakini
chansela
mpya
Leo von Caprivi
alimteua kutembelea
Afrika ya Mashariki ya Kijerumani
na kumpa taarifa kuhusu hali ya eneo hili; koloni iliwahi kuanzishwa na kampuni ya kibinafsi,
Kampuni ya Kijerumani kwa Afrika ya Mashariki
iliyoongozwa na Karl Peters tangu mwaka 1885. Lakini ukali wa kampuni dhidi ya wenyeji wa pwani ulisababisha
uasi mkubwa uliongozwa na Abushiri
na
Bwana Heri
; utawala wa kampuni iliporomoka kabisa na serikali ya Ujerumani ililazimishwa kutuma kikosi cha wanajeshi chini ya
Wissmann
kilichozimia upinzani. Ilhali ilikuwa dhahiri kampuni ya Peters haikuwa na uwezo wa kutawala tena, serikali iliamua kuchukua koloni mkononi mwake na hapo taarifa ya von Soden ilikuwa muhimu.
Tarehe 1 Januari 1891 von Soden alipewa kazi ya kuwa gavana ya kwanza ya
Afrika ya Mashariki ya Kijerumani
alichukua madaraka ambayo hadi wakati ule yalitekelezwa na
kamanda
Wissmann ilhali Wissmann alirudishwa nyumbani kwa sababu aliwahi kuendesha vita mbalimbali na makabila ya ndani na hivyo kuvuka mno mipaka ya makisio yake.
Kati ya shughuli za kwanza Soden alizopaswa kutekeleza ulikuwa uhamisho wa mji mkuu kutoka
Bagamoyo
kuja
Dar es Salaam
na kazi ya kupanga mji mpya.
Hata hivyo, maagizo kwa von Soden yalisema asitumie pesa nyingi mno ajitosheleze na makisio yake; aimarishe utawala juu ya maeneo ya pwani na kukuza biashara. Kuhusu makabila ya ndani alenge kujenga uhusiano nao bila kuingia katika mapigano. Lakini katika nafasi yake hakuwa na mamlaka juu ya jeshi; Soden alikuwa gavana wa kiraia na jeshi la koloni lilikuwa chini ya kamandi ya wanamaji kule Ujerumani.
[2]
1891 kamanda mpya wa
jeshi la Schutztruppe
von Zelewski
[3]
alipanga vita dhidi ya Wahehe chini ya
chifu Mkwawa
; Soden hakuona ulazima wa hatua hiyo lakini alinyamaza kwa sababu makao makuu ilikubali na yeye hakuona hatari. Zelewski alifika Uhehe kwenye Agosti 1891 akaanza kushambulia na kuchoma vijiji. Tarehe 16 Agosti 1891 alipofika Lugalo aliongoza kikosi chake cha askari na wapagazi 500 katika tego lilioandaliwa na Mkwawa; karibu jeshi lote liliangamizwa, wachache tu walirudi kwenye pwani.
Soden alipokea watumwa wa Mkwawa kujadiliana kuhusu amani lakini alimtuma tena
luteni von Prince
kulinda mpaka wa Uhehe. Von Prince aliendelea kuingia ndani ya Uhehe alipoanzisha kituo kipya, bila amri ya von Soden. Mkwawa alijibu kwa kushambulia kituo cha Kondoa mnamo tarehe 6 Oktoba 1892 na kushinda kikosi cha askari 35 chini ya luteni Mjerumani
[4]
. Wakati wa mapigano ya Lugalo kulikuwa pia na ugomvi baina
jeshi la Schutztruppe
na sehemu ya Wachagga kwenye mlima Kilimanjaro; askari mmoja aliwahi kuiba akauawa na luteni kiongozi wa kituo cha Wajerumani huko
Marangu
alikataa upatanisho; baada ya kuuawa kwa akida wa chifu Meli wa Moshi amani ilivunjwa kabisa. Kikosi kidogo cha askari kilichoelekea Moshi ilishambuliwa na Meli kwenye 10 Juni 1892, maafisa 2 Wajerumani kuuawa na wengine walikimbia
[5]
; wajerumani walikosa uwezo wa kufanya chochote dhidi ya Meli hadi mwisho wa 1892.
Katika hali hiyo von Soden aliomba kustaafu akaondoka mwanzo wa 1893.
Von Soden aliishi sasa Ujerumani; alipewa zawadi la shamba kubwa kama shukrani ya serikali hujo Vorra, Bavaria. Hapa alijjenga jumba kubwa na kuwa na nafasi ya mkabaila wa eneo.
Mnamo 1899, von Soden aliitwa kurudi Wurtttemberg ambako alipewa kazi ya katibu mkuu kwenye ofisi ya mfalme.
Mwaka uliofuata alioa mara ya kwanza akifunga ndoa na Helene von Sick (* 5. Februari 1856). Wakati ule alikuwa na umri wa miaka 54. Umri mkubwa wa wenzi wa ndoa labda ilikuwa sababu ya kukosa watoto katika ndoa yao.
Kuanzia mwaka 1900 hadi 1906 alikuwa waziri katika serikali ya ufalme wa Wurttemberg; alisifiwa hasa kwa jitihada za kuongeza njia za reli nchini. 1906 alirudi tena katika kazi ya katibu mkuu wa mfalme aliyotekeleza hadi 1916 alipostaafu baada ya kufikia umri wa miaka 70.
Wakati wa mwisho wa
Vita Kuu ya kwanza ya Dunia
aliona mapinduzi ya Novemba 1918 iliyokomesha ufalme na vyeo vya kikabaila. Mwaka 1920 akiwa na umri wa miaka 74, von Soden alitimiza hamu yake ya kusoma tena. Akajiandikisha kwenye Chuo Kikuu cha Tubingen akaingia katika kozi za
falsafa
,
isimu
na
sanaa
. Miezi michache tu baada ya muhula kuanza, alipata shida ya mwili mnamo Januari 1921, ikifuatiwa na ugonjwa wa siku 14. Julius von Soden alifariki dunia mnamo 2 Februari 1921, siku mbili kabla ya sikukuu ya kuzaliwa kwake kwa miaka 75.
[6]
- ↑
Soden, Julius Freiherr v.
Archived
19 Mei 2016 at the
Wayback Machine
. In:
Deutsches Koloniallexikon
, 1920, Bd. III, S. 369.
- ↑
John Iliffe (1979), A Modern History of Tanganyika, uk. 108
- ↑
Alikuwa
Emil von Zelewski
yeye yule aliyewahi kuwa makala ya Kampuni ya Kijerumani kwa Afrika ya Mashariki huko
Pangani
kwenye mwaka 1888 na kwa ukali wake kuhamasisha wenyeji wa mji huo kupinga utawala wa kampuni.
- ↑
Tom von Prince (1914), Gegen Araber und Wahehe, uk. 182
- ↑
Volkens, Georg (1897): Der Kilimandscharo, uk. 36
- ↑
Nachruf auf Julius von Soden, in: Zeitung des Vereins Deutscher Eisenbahnverwaltung 61 (1921), S. 112.
|
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu
Julius von Soden
kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|