Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Historia ya Polandi
inahusu eneo ambalo leo linaunda
Jamhuri
ya
Polandi
.
Waslavi
walienea kati nchi katika
nusu
ya pili ya
karne ya 5
BK
.
Ukristo
wa
Kikatoliki
kupokewa na
mfalme
Mieszko I
(
960
-
992
) na Wapolandi kwa jumla (
966
) hutazamiwa kama chanzo cha
taifa
lao la pekee katika
jamii
ya Waslavi.
Nchi ilistawi na kuenea hasa chini ya
ukoo
wa
Wajageloni
(
1386
?
1572
).
Katika miaka ya
1569
?
1795
Polandi iliunganishwa na
Lithuania
katika
shirikisho
la kifalme. Mfalme wa Polandi alikuwa pia mtawala wa Lithuania, na tangu
mapatano ya Lublin
nchi hizo mbili zilikuwa na
bunge
la pamoja, lakini kila sehemu iliendelea na
sheria
zake na
jeshi
la pekee. Bunge la pamoja lililokuwa hasa mkutano wa
makabaila
wote lilikuwa na
mamlaka
ya kumchagua mfalme likapata ushawishi mkubwa.
Wagombea wa ufalme waliachana na mamlaka za kifalme wakijaribu kupata
kura
nyingi za wabunge na hivyo nguvu ya dola ilififia.
Mwaka
1764
nchi ilianza kurudi nyuma na zile za jirani, yaani Urusi, Austria na Prussia, ziligawana kwa awamu tatu (
1772
,
1793
,
1795
) eneo lake lote. Yaani kuanzia mwaka
1772
majirani hayo matatu ya Polandi yalivamia shirikisho na kugawana maeneo yake. Kufikia mwaka
1795
maeneo yote yalikwisha kugawiwa kati ya majirani hao.
Wapolandi walijaribu mara kadhaa kujikomboa, lakini walipata
uhuru
kwa muda tu (
1807
-
1815
na
1918
-
1939
).
Wapolandi walijaribu mara kadha kujikomboa, lakini walipata
uhuru
kwa muda tu (
1807
-
1815
na
1918
-
1939
).
Baada ya
vita vikuu vya pili
, Polandi ikawa chini ya utawala wa
Kikomunisti
hadi ilipofaulu kujikomboa (
1989
).
Poland imekuwa nchi mwanachama wa
Umoja wa Ulaya
tangu tarehe
1 Mei
2004
.
Historia ya Ulaya
|
---|
Nchi huru
| |
---|
Nchi zisizokubaliwa
na umma wa kimataifa
| |
---|
Maeneo yanayojitawala
chini ya nchi nyingine
| |
---|
|
|
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu
Historia ya Polandi
kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|