George Corley Wallace Jr. ( 25 Agosti , 1919 ? 13 Septemba , 1998 ) alikuwa mwanasiasa wa Marekani akiwa mwanachama wa Chama cha Kidemokrasia . Alikuwa gavana wa Alabama mara tatu: 1963-1967, 1971-1979 na 1983-1987. Mwaka wa 1968 aligombea urais kama mgombea wa tatu, yaani nje ya vyama vya kawaida, lakini akashindwa na Richard Nixon . Mwaka wa 1972 alijeruhiwa katika shambulio la mauaji akahitaji kutumia kiti cha magurudumu hadi mwisho wa maisha yake.