Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Fransiska wa Roma
(kwa
Kiitalia
Francesca Romana
;
1384
?
9 Machi
1440
) alikuwa
mtawa
kutoka
Roma
,
Italia
.
Ametambuliwa na
Kanisa Katoliki
chini ya
Papa Paulo V
kuwa
mtakatifu
kuanzia
mwaka
wa
1608
.
Tarehe
ya
kifo
chake, yaani
9 Machi
ndiyo
sikukuu
yake
[1]
.
Fransiska alizaliwa katika
mji
wa
Roma
,
Italia
, mwaka 1384.
Aliolewa
mapema mwaka
1396
, akazaa
watoto
watatu. Katika miaka 40 ya ndoa yake alijitokeza kama
mke
na
mama
bora. Alijulikana sana kwa
moyo
wake wa
ibada
,
unyenyekevu
,
upole
,
uvumilivu
na kujitoa kwake mhanga kuwasaidia
maskini
. Aliishi nyakati ngumu, hivyo aliwapatia
mali
yake, na kuuguza
wagonjwa
.
Mwaka
1425
alianzisha
Shirika la Waoblati
waliofuata
Kanuni ya Mt. Benedikto
na baada ya kifo cha
mumewe
akajiunga nao. Alifariki
dunia
mwaka 1440.
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
|
Makala hii bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuiongezea habari
.
|