Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Esikyo wa Antiokia
(alifariki
Antiokia
, leo nchini
Uturuki
,
303
hivi) alikuwa
afisa
wa
jeshi
aliyeuawa kwa kutoswa katika
Mto Oronte
akiwa amefungwa
jiwe
kubwa
mkononi
kwa sababu, wakati wa
dhuluma
ya
kaisari
Dioklesyano
dhidi ya
Ukristo
, alitupa
silaha
zake aliposikia kwamba asiyekubali kutoa
sadaka
kwa
miungu
atapaswa kuacha jeshi
[1]
.
Tangu kale anaheshimiwa na
Wakatoliki
na
Waorthodoksi
kama
mtakatifu
mfiadini
.
Sikukuu
yake huadhimishwa
tarehe
29 Mei
[2]
.
|
Makala hii bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuiongezea habari
.
|