Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ramani
ya dola mnamo mwaka
1700
, lilipofikia kuwa na
eneo
kubwa zaidi, katikati ya
Italia
, mbali ya
miji
ya
Benevento
na
Pontecorvo
Italia kusini
na
wilaya
ya
Venaissin
na mji wa
Avignon
Ufaransa kusini
.
Dola la Papa
lilikuwa
nchi huru
chini ya
himaya
ya
Papa
kuanzia
miaka ya 700
hadi
1870
.
Chanzo chake ni
uvamizi
wa ma
kabila
ya
Wagermanik
uliobomoa
Dola la Roma
upande wa
magharibi
wa
Bahari ya Kati
. Wenyeji, wengi wao wakiwa
Wakristo
Wakatoliki
, walimkimbilia Papa kama kiongozi wao atakayeweza kuwasaidia katika matatizo.
Baadaye
Wafaranki
walikubali kumuachia Papa
mamlaka
ya kisiasa juu ya maeneo mbalimbali nje ya Roma. Polepole maeneo yaliongezwa hata kufikia mikoa 3 na nusu ya Italia ya leo:
Lazio
,
Umbria
,
Marche
na sehemu ya
Emilia-Romagna
.
Dola lilikoma tarehe
20 Septemba
1870,
jeshi
la
Italia
lilipoteka
mkoa
na
mji
wa
Roma
, isipokuwa
mtaa
wa
Vatikano
.
Kwa mapatano ya tarehe
11 Februari
1929
, badala yake ilianzishwa
Mji wa Vatikani
, nchi ndogo kuliko zote
duniani
(
kilometa mraba
0.44, wakazi 600 hivi), lakini huru ili
mamlaka
ya kiroho ya Papa isiingiliwe na
watawala
wa
dunia
kama ilivyotokea zamani.
|
Makala hii kuhusu Kanisa Katoliki bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu
Dola la Papa
kama historia yake au maelezo zaidi?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|