Dini za wananchi wengi wa nchi ya Tanzania
ni
Uislamu
,
Ukristo
na
dini asilia za Afrika
(
dini za jadi
). Nje ya hao wako wachache wanaofuata
Uhindu
,
Usikh
na
dini
nyingine na mara nyingi hawa ni
wahamiaji
katika nchi au wamezaliwa katika vikundi vyenye asili ya
uhamiaji
kutoka nje.
Siasa
ya
serikali
na
dola
ni kutokuwa na
dini rasmi
.
Katiba
inatoa
uhuru wa dini
, na serikali inaheshimu
haki
hii kwa vitendo.
Hadi vizazi vichache vilivyopita idadi kubwa ya wakazi wa eneo la
Tanzania
ya leo walifuata dini asilia za Kiafrika.
Wakati wa
karne ya 19
Uislamu ulipatikana kwenye
pwani
hasa katika
mazingira
ya miji ya
Waswahili
na pia kwenye vituo vya
biashara
vya Waswahili kando ya
njia
ya misafara kuelekea
nchi za Maziwa Makuu
(Viktoria, Tanganyika n.k.) kutoka pwani.
Tangu katikati ya karne ya 19
wamisionari
Wakristo wa kwanza walianza kufika kwenye pwani na kujenga vituo vyao
barani
.
Wakristo na Waislamu walikuta kote wafuasi wa dini za jadi. Polepole wengi wao walihamia upande wa dini hizo kubwa. Lakini
desturi
na
ibada
mbalimbali za
jadi
ziliendelea kufuatwa na sehemu ya Wakristo na Waislamu wapya hadi leo.
Asilimia tisini na saba ya wakazi wa
funguvisiwa
vya
Zanzibar
ni Waislamu. Kwa upande wa
Tanzania bara
, jumuia za Kiislamu huzingatiwa sana katika maeneo ya pwani, na baadhi ya Waislamu wanaoishi katika maeneo ya mijini huko bara.
Kati ya asilimia 80 na 90 ya idadi ya Waislamu nchini ni
Sunni
wa
madhhab
ya
Shafi'i
. Wasunni wachache wenye asili ya
Asia
ni
Wahanbali
, kuna pia wafuasi
Maliki
na
Hanbali
ambao wana asili ya
Yemen
.
Washia
ni wachache, wengi wao ni wenye asili ya Asia au
Uarabuni
. Kundi linaloonekana zaidi ni
Ismaili
au wafuasi wa
Aga Khan
ambao ni kitengo cha
Washia Sabi'a
. Kitengo kingine cha Shia hii ni
Bohra
. Wafuasi wa
Shia Ithnasheri
(Imami) si wengi, lakini wanapata usaidizi kutoka
Uajemi
ambako
imani
yao ni dini rasmi.
Wafuasi wa
Ibadiyya
wana asili ya
Oman
.
Kundi la
Ahmadiyya
liko, wanajitahidi kupata waumini wapya lakini bila mafanikio makubwa.
Idadi ya
madhehebu
ya Kikristo inajumlisha
Kanisa Katoliki
,
Waprotestanti
wa aina mbalimbali (
Walutheri
,
Wapentekoste
,
Waanglikana
,
Wamoravian
,
Wasabato
,
Wameno
,
Kanisa Jipya la Kitume
n.k.),
Waorthodoksi
na
Waorthodoksi wa Mashariki
wachache, mbali ya
Wamormoni
na
Mashahidi wa Yehova
ambao mara nyingi hawahesabiwi na madhehebu hayo kuwa Wakristo kwa sababu ya kutosadiki
umungu
wa
Yesu
.
Kuna Watanzania wanaofuata
Uhindu
na
Usikh
, hasa
wageni
na
raia
wenye asili ya
Asia
.
Imani
ya
Baha'i
nayo imeanzishwa katika maeneo kadhaa ya nchi.
Takwimu ya
dini nchini
Tanzania
kwa sasa haipatikani kwa sababu maswali kuhusu dini yaliondolewa na serikali katika sensa baada ya mwaka
1967
. Sensa ile ya tarehe
27 Agosti
ilihesabu wafuasi wa dini za jadi kuwa 34.3%, Wakristo 33.5% na Waislamu 31.4%, mbali na wengineo 0.8%.
[1]
Tangu mwaka ule swali la takwimu ya kidini Tanzania limejadiliwa sana inaonekana ni swali lenye uzito wa kisiasa pamoja na upande wake wa kitaalamu.
Kwa miaka mingi makadirio ya kawaida yalikuwa Watanzania ni theluthi 1 wafuasi wa dini za jadi, theluthi 1 Waislamu na theluthi 1 Wakristo.
[2]
Lakini ni wazi ya kwamba dadi ya wafuasi wa dini za jadi imeendelea kupungua. Baadhi ya viongozi na wanaelimu-jamii wanakadiria kwamba jumuia za
Kikristo
na
Kiislamu
zipo sawa tu kwa ukubwa, zote huhesabiwa kiasi cha asilimia 30 hadi 40 kwa idadi ya wakazi, na waliosalia ni waumini wa
imani
zingine,
dini za jadi
, na wale wasio na
dini
kabisa.
Lakini wataalamu wengine wanasema uwiano huo unashikiliwa kisiasa kwa sababu uhusiano kati ya Wakristo na Waislamu ni jambo la siasa ya taifa kwa hiyo makadirio yanaelekea kutaja uwiano sawa kati ya pande hizi mbili.
[3]
Kwa hiyo namba zote kuhusu takwimu ya dini nchini Tanzania ni makadirio tu hakuna namba za kutegemea. Vyanzo vinavyotaja namba vinatofautiana sana mara nyingi kufuatana dini ya wahariri.
- "World Christian Encyclopedia" (toleo la pili, Oxford 2001) imekadiria kwa mwaka 2000 Wakristo kuwa 50.4 % (Wakatoliki 24.7%, Waprotestanti mbalimbali 16.5%, Waanglikana 7.9%, wasio na madhehebu maalumu 3.5%, madhehebu huru 1.9%, madhehebu yasiyokubali imani ya msingi ya Wakristo wengine wote 0.1%, wenye kufuata madhehebu mawili kwa wakati mmoja 4.2%), Waislamu 31.8%, wafuasi wa dini za jadi 16.1% na wengineo 1.8%. Pia imetabiria kwa mwaka
2025
uwiano kuwa 56.1, 32.8, 8.9 na 2.1%, na kwamba kufikia mwaka
2050
Wakristo na Waislamu watakuwa karibu 65 na 35% kati ya wakazi wa nchi.
- Takwimu zinazoonyeshwa na Waislamu hudai kundi kubwa la Watanzania kuwa Waislamu wakiwa na asilimia 50 - 60 za watu wa nchi
[5]
- Kuna shirika za Kiislamu zinazotabiri Tanzania itakuwa nchi ya Waislamu wengi mnamo mwaka 2020
[6]
Pande zote zinarejea takwimu za kuongezeka za watu katika maeneo fulani wakiongeza makadirio yao juu ya matokeo kwenye namba za kidini.
[7]
- ↑
International Religious Freedom Report 2007: Tanzania
. United States
Bureau of Democracy, Human Rights and Labor
(14 Septemba 2007).
This article incorporates text from this source, which is in the
public domain
.
- ↑
linganisha ukurasa wa gazeti The Citizen kuhusu Tanzania - Country Profile - TANZANIA - RELIGIONS
http://www.thecitizen.co.tz/about-tanzania.html?start=8
Archived
24 Desemba 2010 at the
Wayback Machine
.
- ↑
Kuna taarifa zisizothebitshwa juu ya ripoti moja ya serikali ya mwaka 1990, ambayo haikusambazwa zaidi, ilionyesha Ukristo unavyozidi kuongezeka kasi kuliko Uislamu, kwa kupata wafuasi hasa kutoka dini za jadi ambazo kwa wakati huo zilikuwa zinaongoza tu katika mkoa wa
Shinyanga
. Mkoa wa
Iringa
ulionekana kuongoza kwa wingi wa Wakristo (91%) na uchache wa Waislamu (2%), mbali na wafuasi wa dini za jadi kuwa 7%. Mikoa ya Kiprotestanti ilikuwa hasa
Mbeya
na
Dodoma
. Wakatoliki walikuwa wengi hasa katika mkoa wa
Rukwa
na
Kagera
.
- ↑
[1]
- ↑
linganisha
Tovuti ya Muslim Population Worldwide inadai asilimia 55 Waislamu mwaka 2008
na
M. Amir Ali Muslim Population Statistics: Tanzania 50% = watu 18,722,696
na
Lodi, Nordic Journal of African Studies 3(1): 88?98 (1994)- uk. 91
- ↑
"Nakala iliyohifadhiwa"
. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka
chanzo
mnamo 2020-02-17
. Iliwekwa mnamo
2010-12-06
.
- ↑
Mfano wa makadirio ya wataalamu wanoona Wakristo mbele ni hivi Sababu ya ongezeko la kasi la Wakristo linatokana na wafuasi wa dini wa jadi, na hasa watoto wao, kuelekea zaidi Ukristo. Pia makabila ya pwani na ya jijini kuzaa kidogo kuliko wakazi wa mikoa ya bara, hasa Tanzania Magharibi ambayo katika sensa ya mwaka
2002
ilionyesha ongezeko kubwa zaidi.