Chingis Khan
(pia:
Genghis Khan
; takriban
1162
?
18 Agosti
1227
) alikuwa
kiongozi
wa
Wamongolia
aliyeunda
Milki ya Wamongolia
iliyoendelea kutawala eneo kubwa kuanzia
China
pamoja na
Asia ya Kati
hadi
Urusi
na
Mashariki ya Kati
.
Kuunganisha makabila ya Wamongolia
[
hariri
|
hariri chanzo
]
Alizaliwa kwa
jina
la
Temujin
kama
mtoto
wa
chifu
wa
kabila
la Kimongolia. Wakati ule Wamongolia walikuwa
wafugaji
wahamaji
walioishi kaskazini mwa nchi ya
Mongolia
ya leo. Walikuwa na makabila mengi yaliyoendelea kupigana kwa
vita
. Temujin alishiriki katika vita vingi akaendelea kuunganisha makabila mbalimbali. Tangu
mwaka
1201
alikuwa na nguvu ya kutosha akashambulia
mataifa
ya jirani kama
Watartari
waliowahi kumwua baba yake akawashinda. Mwaka
1206
Temujin aliitisha mkutano wa viongozi wote wa Wamongolia waliomkubalia kama kiongozi mkuu na kumpa
cheo
cha "Chingis Khan" yaani
mtawala
mkubwa.
Maazimio ya mkutano yalianzisha
dola
jipya ambamo Temujin alikuwa mtawala pekee mwenye
madaraka
ya kutunga
sheria
. Alitawala kwa msaada wa
halmashauri
iliyokuwa na
mama
yake,
kaka
yake na wana wake. Temujin alimwagiza mwana wake aliyejua
mwandishi
kuandika sheria zote za kale zilizohifadhiwa kwa
kumbukumbu
tu katika
kitabu
pamoja na
amri
na sheria mpya alizoendelea kutangaza. Nakala za kitabu hicho zilitumwa katika pande zote za milki yake. Sheria hizo zilimaliza utawala wa machifu waliowahi kuamua mambo kufuatana na
hiari
zao.
Temujin aliendelea kuanzisha
jeshi
kwa kutangaza sheria kuwa kila Mmongolia alipaswa kuwa
mwanajeshi
. Aliweza kuzawadia
askari
wake kwa
mali
zilizotekwa vitani. Yeye mwenyewe aliteua viongozi waliosimamia vikosi vya wanajeshi 1,000. Hapo hakuteua tena
ndugu
zake bali aliwachagua viongozi hao kulingana na uwezo na uaminifu.
Mwenyewe alikuwa na kikosi cha ulinzi wake wa wanajeshi wateule 10,000.
Kazi kubwa ya Temujin ilikuwa kujenga
umoja
na nidhamu. Wamogolia walizoea kuungana kwa vita lakini kuacha maungano na kufarakana kufuatana na hiari za machifu. Kwa kuunda jeshi la pamoja Temujin alikuwa na chombo cha kuunganisha makabila kwa njia ya kudumu kwa sababu machifu wa kale hawakuwa na nafasi tena katika muundo huo wakapungukiwa umuhimu.
Baada ya kutwaa milki za majirani alipata pia maafisa
Wachina
hasa waliokuwa na maarifa ya utawala, hivyo aliweza kuanzisha utaratibu wa
kodi
na
huduma
.
Mwenyewe hakujua kuandika wala kusoma lakini alielewa umuhimu wa
maandiko
akaamuru kutungwa kwa
mwandiko
maalumu kwa ajili ya
lugha
ya
Kimongolia
.
Baada ya kuimarisha utawala wake kati ya
China
na
Bahari ya Kaspi
alijenga
mji mkuu
mpya wa
Karakorum
uliokuwa mji wa kwanza wa kudumu wa Mongolia. Kwa kazi kama utawala,
biashara
na
ufundi
alichukua watu kutoka sehemu mbalimbali za milki yake; alitambua ya kwamba Wamongolia wenyewe walizoea
ufugaji
na vita tu kwa hiyo alitegemea
wafanyabiashara
Waislamu
Waturuki
na
Waajemi
, maafisa wa utawala na mafundi Wachina na
wataalamu
Wakristo
.
Baada ya kuunganisha makabila ya wafugaji Temujin aliongoza jeshi lake dhidi ya milki ya China katika kusini. Kuanzia mwaka
1211
alivuka
ukuta mkubwa wa China
kwa jeshi la askari 100,000. Mwaka
1215
alitwaa
Beijing
na kuanzia 1219 hata milki ya
Korea
ilianza kumlipia hongo.
Mwaka
1218
kulitokea matatizo na majirani wa
Khorezmu
upande wa
magharibi
;
msafara
wa Kimongolia uliwahi kushambuliwa na mabalozi waliotumwa huku kupeleleza hali waliuawa. Kwa hiyo Temujin aliitisha mkutano wa viongozi wa milki yake wakaamua kushambulia Khorezmu. Mkutano uleule ulimkubali pia mwana wa tatu Ugedai kama mrithi wa Temujin atakayemfuata kama Khan mkuu.
Miaka
1219
/
1220
Wamongolia walimshinda
mfalme
wa Khorezmu wakaangamiza
miji
ya ufalme huu na kuua watu wengi. Vikosi vya jeshi hilo viliendelea upande wa magharibi na kuangamiza nchi za
Warusi
na sehemu za
Kaukazi
.
Mwaka 1227 Chingis Khan alikufa akiwa
mzee
; wengine husema ya kwamba sababu ya
kifo
ilikuwa anguko kutoka juu ya
farasi
; wengine husema ya kwamba
binti
wa mfalme aliyeuawa na Temujin alilipiza
kisasi
kwa kumchoma kwa
kisu
.
Kaburi
lake lilifichwa na walinzi wake kufuatana na
desturi
ya Wamongolia haijajulikana hadi leo. Inasemekana ya kwamba
wapandafarasi
1,000 walikanyaga sehemu ya kaburi kwa
miguu
ya farasi zao halafu waliuawa wenyewe baada ya kuleta
taarifa
ya kwamba walitimiza kazi ya kumzika Chingis Khan.
Wafuasi wake waliendela kupanua milki. China yote pamoja na Urusi zilikuwa majimbo ya milki ya Wamongolia nayo ilikuwa milki kubwa katika
historia
ya
dunia
.
Kwa watu wengi Chingis Khan ni sawa na ushindi katili na wa kinyama.
Lakhi
za watu waliuawa na wanajeshi wake. Aliposhinda taifa la Watartari aliamuru watu wote wenye
urefu
juu ya
futi
nne wauawe yaani watu wazima wote. Wamongolia siku hizi wanamwona kama Baba wa Taifa lao. Alitumia miaka mingi kuunganisha na kueneza makabila ya watu wahamaji wa Mongolia.
Baadhi ya
wanahistoria
wanasema kwamba alikuwa na
kichwa
kizuri cha kijeshi kuliko karibu watu wote wengine katika historia ya dunia.
|
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu
Chingis Khan
kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|