Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
'
Binyavanga Wainaina
(
18 Januari
1971
-
21 Mei
2019
) alikuwa
mwandishi
kutoka nchini
Kenya
.
Alizaliwa
Nakuru
, nchini
Kenya
. Alihudhuria
masomo ya msingi
na
sekondari
nchini Kenya kabla ya kujiunga na
Chuo Kikuu cha Transkei
,
Afrika Kusini
.
Baada ya kumaliza masomo yake alihamia katika
jiji
la
Cape Town
ambapo alifanya
kazi
kama mwandishi wa kujitegemea wa masuala ya
chakula
na
utalii
.
Mwezi
Julai
2002
Binyavanga alishinda
Tuzo ya Caine
kwa
Uandishi wa Kiafrika
. Yeye ndiye
mwanzilishi
wa
jarida
la
fasihi
la
Kwani?
, ambalo linachukuliwa kuwa ndio
gazeti
kuu la masuala ya fasihi toka
Afrika Mashariki
.
Aliaandika
riwaya
yake ya kwanza iitwayo
The Fallen World of Appearances
. Mwaka
2003
alipata
tuzo
toka
Chama cha Wachapishaji wa Kenya
(Kenya Publishers Association) kutokana na juhudi zake za kuendeleza fasihi ya Kenya.
Alisomea
shahada
ya pili ya
Uandishi wa Ubunifu
katika
Chuo Kikuu cha East Anglia
. Kazi zake zimetoka katika magazeti na majarida mbalimbali kama vile
National Geographic
,
The East African
,
The Sunday Times
(ya
Afrika Kusini
),
The Guardian
(ya
Uingereza
).
Baadhi ya kazi alizoandika ni:
- Discovering Home
(
Hadithi fupi
, G21Net, 2001)
- An Affair to Dismember
(Hadithi fupi)
- Beyond the River Yei: Life in the Land Where Sleeping is a Disease
(Riwaya ya picha pamoja na
Steven Torfinn
,
Kwani Trust
).
Tarehe
1 Disemba
2016
, katika
siku ya UKIMWI Duniani
, Wainaina alitangaza kupitia
akaunti
yake ya
Twitter
kwamba amethibitika kuwa na
UKIMWI
.
[1]
Wainaina amefariki
dunia
baada ya kupata
ugonjwa
majira ya saa nne
usiku
ya tarehe 21 Mei, 2019, katika Hospitali ya Aga Khan jijini
Nairobi
, hiyo ni kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa wanandugu.
[2]