Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Baisikeli
(kwa kawaida
baiskeli
; pia
basikeli
; kutoka
Kilatini
"bis", "mara mbili" na
Kigiriki
"κ?κλο?", kyuklos, "
duara
" kupitia
Kifaransa
/
Kiingereza
"bicycle") ni
chombo
cha
usafiri
kinachoendeshwa kwa
nguvu
ya
misuli
ya
binadamu
.
Baisikeli huwa na ma
gurudumu
mawili yanayoshikwa na
fremu
,
kiti
kimoja,
kanyagio
,
breki
na
usukani
.
Tabia
nyingine za kawaida ni kuwa na
taa
mbele na nyuma. Baisikeli bora huwa pia na
gia
zinazorahisisha kazi ya kukanyaga kanyagio.
Kwa kawaida nguvu hupelekwa kwa
nyororo
kutoka kanyagio kwenda gurudumu la nyuma. Magurudumu huwa na ma
tairi
yaliyojaa
hewa
.
Katika nchi nyingi baisikeli ni chombo muhimu cha usafiri. Zamani baisikeli ilikuwa usafiri wa
maskini
lakini pia katika
nchi kadhaa zilizoendelea
watu hutumia baisikeli ama kwa usafiri wa
mjini
au kwa
burudani
.
Sayansi
imegundua ya kwamba baisikeli ni usafiri wa
haraka
mjini katika
umbali
wa
kilomita
chache. Katika nchi nyingi kuna njia za pekee kwa ajili ya baisikeli kando ya
barabara
ya ma
gari
.
Baisikeli ni usafiri unaotumia
nishati
kidogo na hivyo kuwa
nafuu
kwa
hifadhi ya mazingira
.
Mashindano ya baisikeli
ni
tawi
muhimu la
michezo
ya kimataifa.
Aina ya pekee ya baiskeli hutengenezwa kwa magurudumu matatu (kwa
Kiingereza
tricycle
). Mara nyingi kuna gurudumu
moja
mbele sawa na baisikeli ya kawaida na magurudumu mawili nyuma, lakini
muundo
wa kinyume hutumiwa pia.
- baisikeli za
watoto
na watu wenye matatizo (kama
wazee
) ya kuendesha baisikeli ya kawaida huwa na magurudumu matatu kwa sababu si rahisi kuanguka.
- baisikeli za kubeba
mizigo
au
abiria
hutengenezwa mara nyingi kwa magurudumu matatu maana ni thabiti zaidi.
Hivyo magari ya kubeba abiria aina ya
riksha
yaliendelezwa kuwa riksha ya baisikeli iliyoendelea kuwa mtangulizi wa
bajaji
.
-
Usalama kwa watoto
-
Mwuza magazeti
-
-
|
Makala hii kuhusu mambo ya
teknolojia
bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu mada hiyo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|