Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Shirika la Mkombozi Mtakatifu sana
(kwa [[Kilatini:
Congregatio Sanctissimi Redemptoris
? Ufupisho: C.Ss.R au CSSR) ni shirika la kitawa la kimisionari la
Kanisa Katoliki
lililoanzishwa na
Alfonso Maria wa Liguori
tarehe
9 Novemba
1732
huko
Scala
(karibu na
Amalfi
,
Italia
) ili kushughulikia watu waliosahaulika wa mkoa wa
Napoli
.
Kwa
Kiingereza
wanashirika wanajulikana kama
Redemptorists
. Wakiwa mapadri na mabradha wanafanya kazi katika nchi zaidi ya 77 duniani kote. Mkuu wao anaitwa Michael Brehl.