Alizaliwa tarehe 26 Agosti 1910 mjini
Skopje
(katika
Dola la Kituruki
, leo
mji mkuu
wa
Makedonia Kaskazini
) katika
familia
ya
Waalbania
akaitwa
Agnes Gonxha Bojaxhiu
. Alizaliwa katika familia ya Kikatoliki na
alibatizwa
siku moja baada ya kuzaliwa, yaani tarehe
27 Agosti
1910 na siku hiyo aliyobatizwa aliitazama siku zote kama siku yake ya kuzaliwa rasmi.
[3]
Alipofikia
umri
wa miaka 18 alijiunga na shirika la
Masista wa Loreto
huko
Ireland
na mwaka
1929
alitumwa Uhindi kufanya utume wake kama
mmisionari
afundishe kwenye
shule
ya masista mjini Kolkata alipoendelea hata kuwa
mkuu wa shule
.
Hata hivyo aliguswa sana na hali ya ma
fukara
nje ya shule akajaliwa
neema
ya wito wa pekee yaani kujitoa kwa ajili ya watu maskini sana na wale ambao jamii imewatenga, kwa kuwasaidia na kuishi pamoja nao. Wito huu mpya ulikuwa chanzo cha Shirika la Masista Wamisionari wa Upendo lililoanza rasmi mnamo
7 Oktoba
1950
.
[4]
Na sasa limeenea sehemu mbalimbali duniani likiendeleza utume wa Mama Tereza.
Kwa kibali cha wakuu wa shirika lake na wa
Kanisa
mwaka
1948
alitoka
jumuiya
ya Loreto akaanzisha
maisha
duni kati ya wakazi wa
mitaa ya vibanda
.
Alianzisha shule lakini baada ya muda alitambua umuhimu wa kuzingatia zaidi hali ya watu ambao walikuwa
wagonjwa
na hatimaye kufa katika mitaa hiyo.
Mwaka
1950
alianzisha shirika la Masista
Wamisionari wa Upendo
ambalo mwanzoni lilikuwa jumuiya ndogo ya masista 12 tu.
Kati ya kazi zao za kwanza ilikuwa
nyumba
kwa watu
mahututi
; masista waliwakusanya wakiwa wamelala
barabarani
na kuwapeleka katika nyumba hiyo walipopata
dawa
,
chakula
na usaidizi mwingine.
Shirika lilikua haraka sana; hadi leo kuna masista 4,500 kwa jumla katika matawi mengi kote
duniani
.
Wanaendesha nyumba kwa
watoto
yatima
, wagonjwa wa
UKIMWI
, wenye
ukoma
,
walemavu
,
walevi
, wenye
kichaa
na kila aina ya matatizo maishani.
Mwaka
1979
alipewa
Tuzo ya Nobel ya Amani
ambayo hutolewa na
Umoja wa Mataifa
kwa sababu jumuiya ya kimataifa iliweza kutambua mchango wake katika kutetetea
haki
za wanyonge.
[5]
. Mama huyu ni mfano halisi wa namna ya kuishi kama
binadamu
kwa sababu kila mwanadamu ni sura na mfano wa Mungu, hivyo kuwajali na kuwasaidia wale wasiojiweza na wale ambao kamwe hawawezi kurudisha kwetu chochote, huwasaidia watu hao kuiona sura halisi ya Mungu kupitia sisi. Kwa kweli
maisha
yake yalikuwa ushuhuda halisi wa
upendo
wa
Mungu
hapa duniani. Pia Mama Tereza ni mfano halisi wa kuishi kama
Mkristo
kwa sababu hata
Kristo
mwenyewe alijitoa kwa ajili ya wale ambao jamii haikuwathamini kwa kipindi kile ambao ni wachungaji,
wavuvi
, watoza ushuru na wenye dhambi, hivyo kujitoa kwa ajili ya wale wasiojiweza au wale ambao jamii haiwathamini tena inawasaidia wao kumwona na kumtambua Kristo kupitia sisi na huwawezesha kuuona uwezo mkuu wa Mungu kupitia matukio ya maisha yao.
Mnamo mwaka
1990
aling'atuka kuongoza shirika lake kama mkuu wa shirika kimataifa.
Alifariki akiwa na
umri
wa miaka 87 huko Calcutta,
Bengal Magharibi
nchini India tarehe 5 Septemba 1997 akafanyiwa
mazishi
ya kitaifa.
Baba yetu, mwanao nipo hapa, tayari kwako
unitumie ili kuendelea kupenda ulimwengu kwa kuupatia Yesu
na, kwa njia yangu, kumtoa kwa kila mmoja na kwa ulimwengu.
Ee Bwana, utufanye tustahili kutumikia watu wenzetu
ambao ulimwenguni kote wanaishi na kufa kwa ufukara na njaa.
Kwa mikono yetu uwape leo mkate wao wa kila siku;
na kwa upendo wetu wenye kuelewa uwape amani na furaha.
Ee Bwana wangu, nakupenda,
Mungu wangu, najuta,
Mungu wangu, nakuamini,
Mungu wangu, nakutumainia.
Utusaidie kupendana unavyotupenda.
Bwana Yesu, wewe ambaye uliumba kwa upendo,
ulizaliwa kwa upendo, ulitumikia kwa upendo, ulitenda kwa upendo,
uliheshimiwa kwa upendo, uliteseka kwa upendo,
ulikufa kwa upendo, ulifufuka kwa upendo,
nakushukuru kwa upendo wako kwangu na kwa ulimwengu wote,
na kila siku nakuomba: unifundishe mimi pia kupenda!
Amina.
Baada ya kifo chake maandishi yake yaliyotolewa hadharani yakafichua
siri
ya maisha yake ya ndani, yaani kwamba alipitia kwa karibu miaka 50 mfululizo katika hali ngumu inayoitwa
usiku wa roho
, bila ya hiyo kuweza kumzuia atabasamu muda wote.
- Teresa, Mother et al.,
Mother Teresa: In My Own Words
. Gramercy Books, 1997.
ISBN 0-517-20169-0
.
- Teresa, Mother & Kolodiejchuk, Brian,
Mother Teresa: Come Be My Light
, New York: Doubleday, 2007.
ISBN 0-385-52037-9
.
- Chawla, Navin.
Mother Teresa
. Rockport, Mass: Element Books, 1996.
ISBN 1-85230-911-3
- Chawla, Navin.
Mother Teresa: The Authorized Biography
, Diane Pub Co. (Machi 1992),
ISBN 978-0-7567-5548-5
. First published by Sinclair-Stevenson, U.K. (1992), since translated into 14 languages in India and abroad.
Indian language
editions include
Hindi
,
Bengali
,
Gujarati
,
Malayalam
,
Tamil
,
Telugu
, and
Kannada
. The foreign language editions include
French
,
German
,
Dutch
,
Spanish
,
Italian
,
Polish
,
Japanese
, and
Thai
. In both Indian and foreign languages, there have been multiple editions. The bulk of royalty income goes to charity.
- Chawla, Navin.
The miracle of faith
, article in the Hindu dated 25 Agosti 2007
" The miracle of faith
"
Archived
4 Novemba 2007 at the
Wayback Machine
.
- Chawla, Navin.
Memories of Mother Teresa
, article in the Hindu dated 26 Agosti 2006
" Memories of Mother Teresa
"
Archived
23 Mei 2011 at the
Wayback Machine
.
- Chawla, Navin. Touch the Poor... ? article in India Today dated 15 Septemba 1997
" Touch the Poor...
"
Archived
3 Septemba 2010 at the
Wayback Machine
.
- Chawla, Navin.
The path to Sainthood
, article in The Hindu dated Saturday, 4 Oktoba 2003
" The path to Sainthood
"
Archived
2 Desemba 2008 at the
Wayback Machine
.
- Chawla, Navin.
In the shadow of a saint
, article in
The Indian Express
dated Septemba, 05, 2007
" In the shadow of a saint
"
Archived
2 Desemba 2008 at the
Wayback Machine
.
- Chawla, Navin.
Mother Teresa and the joy of giving
, article in
The Hindu
dated 26 Agosti 2008
" Mother Teresa and the joy of giving
"
Archived
28 Agosti 2008 at the
Wayback Machine
.
- Donohue, William A.
Unmasking Mother Teresa’s Critics
, Sophia Institute Press2016)
- Eileen Egan
and Kathleen Egan, OSB.
Prayertimes with Mother Teresa: A New Adventure in Prayer
,
Doubleday
, 1989.
ISBN 978-0-385-26231-6
.
- Gonzalez-Balado, Jose Luis
Mother Teresa: in my own words
, Gramercy Book, New York, 1997,
ISBN 0-517-20169-0
- Christopher Hitchens
,
The Missionary Position: Mother Teresa in Theory and Practice, Verso, 1995, ISBN|1-85984-054-X. Plus a debate in the
New York Review of Books
:
Defense of Mother Teresa
,
Hitchens' answer
,
Leys' reply
.
- Johnson, Mary
An Unquenchable Thirst: Following Mother Teresa in Search of Love, Service, and an Authentic Life
, 2011,
ISBN 978-0385527477
- Le Joly, Edward.
Mother Teresa of Calcutta
. San Francisco: Harper & Row, 1983.
ISBN 0-06-065217-9
.
- Muggeridge, Malcolm
.
Something Beautiful for God.
ISBN 0-06-066043-0
.
- Muntaykkal, T.T.
Blessed Mother Teresa: Her Journey to Your Heart
.
ISBN 1-903650-61-5
.
ISBN 0-7648-1110-X
.
"Book Review"
. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka
chanzo
mnamo 2006-02-09
. Iliwekwa mnamo
2012-06-24
.
.
- Scott, David.
A Revolution of Love: The Meaning of Mother Teresa
. Chicago: Loyola Press, 2005.
ISBN 0-8294-2031-2
.
- Spink, Kathryn.
Mother Teresa: A Complete Authorized Biography
. New York: HarperCollins, 1997.
ISBN 0-06-250825-3
- [1]
- Kolkata Mother Teresa Information
Archived
1 Februari 2014 at the
Wayback Machine
.
- Tovuti ya jumuiya za Mama Teresa
Archived
27 Desemba 2007 at the
Wayback Machine
.
- Mother Teresa of Calcutta Center, India ? Official Site
- Missionaries of Charity Brothers (Active Branch)
- Mother Teresa and her patron saint, St. Therese of Lisieux
Archived
7 Oktoba 2020 at the
Wayback Machine
.
- Mother Teresa Memorial Page
- Mother Teresa Gallery
Archived
19 Agosti 2012 at the
Wayback Machine
.
- Mother Teresa Women`s University, Kodaikanal, Tamil Nadu, India ? Official site
- Nobel Laureate Biography (Nobel Foundation)
- Mother Teresa's 1979 Nobel Peace Prize acceptance speech
- Complete Mother Teresa Quotations
- The TIME 100: The Most Important People of the Century ? Mother Teresa
Archived
1 Mei 2009 at the
Wayback Machine
.
- Missionaries of Charity Fathers (MC Fathers / MC Priests) ? Official Website: Biography of Mother Teresa
Archived
30 Septemba 2012 at the
Wayback Machine
.
- Mother Teresa's Crisis of Faith (TIME.com)
Archived
16 Agosti 2013 at the
Wayback Machine
.
- Speech at National Prayer Breakfast, Washington, D.C. 3 February 1994
- Peggy Noonan, "Still, Small Voice,"
Crisis
, 1 February 1998
Archived
23 Agosti 2006 at the
Wayback Machine
. (account of the National Prayer Breakfast speech)
- Mother Teresa
at the
Internet Movie Database
- Missionaries of Charity Active and Contemplative Sisters with U.S. contact information (CMSWR member page)
Archived
19 Agosti 2007 at the
Wayback Machine
.
- India to give Mother Teresa state funeral
,
CNN
- Mother Teresa
, Encyclopædia Britannica
- "Mother Teresa, John Paul II, and the Fast-Track Saints"
Archived
24 Aprili 2012 at the
Wayback Machine
. by
Michael Parenti
, CommonDreams.org, 22 Oktoba 2007
- Biography: Mother Teresa
|
Makala hii bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuiongezea habari
.
|