Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kalenda ya Kichina
ni
kalenda
ya kidesturi inayoitwa pia
kalenda ya Han
. Inatumiwa nchini China na pia na watu wanaofuata utamaduni wa kichina penginepo duniani pamoja na
Kalenda ya Gregori
.
Mambo ya serikali na mipango ya kiuchumi hufuata kalenda ya Gregori. Lakini sikukuu za kidesturi zinafuata kalenda ya Kichina, kwa mfano mwaka mpya wa Kichina. Kalenda hii hutumiwa pia kwa kupanga tarehe za arusi, mazishi au kuhamia nyumba kwa sababu Wachina wengi huamini kuna tofauti kati ya siku za bahati nzuri na bahati mbaya.
Kalenda wa Kichina inafuata mwendo wa
mwezi
pamoja na mwendo wa
jua
kwa hiyo inaunganisha tabia za
kalenda ya mwezi
na
kalenda ya jua
.
Kwa kawaida mwaka mmoja huwa na miezi 12 lakini kuna pia miaka yenye miezi 13 - hii inatokea mara saba katika kila kipindi cha miaka 19. Kila mwezi unaanza kwenye siku ya
mwezi mwandamu
.
Muda wa mwaka wa kawaida ni siku 353 - 355. Kama ni mwaka una miezi 13, muda wake ni siku 383 - 385.
Mwaka mpya hutokea kati ya Januari 21 na Februari 21.
|
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu
Kalenda ya Kichina
kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|