Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Florida
ni
jimbo
la
Marekani
la kujitawala katika kusini mashariki ya nchi. Umbo lake ni rasi inayoanza Marekani bara kuelekea
Kuba
. Upande wa magharibi ni maji ya
ghuba ya Meksiko
na upande wa mashariki maji ya
Atlantiki
. Upana wa rasi ni kati ya 160 hadi 200 km; upande wa kaskazini kabisa eneo la jimbo lapanuka kama kanda mwambaono wa ghuba ya Meksiko.
Florida imepakana na majimbo ya Marekani ya
Georgia
na
Alabama
. Nchi za
Karibi
za
Kuba
na
Bahamas
ni karibu.
Jina la Florida ni ya
Kihispania
, maana yake ni "yenye maua".
Florida ina eneo la 137,374 km², ni nafasi ya 22 kati ya majimbo ya Marekani. Upande wa kusini wa rasi kuna kundi la visiwa la "Florida Keys" lenye umbo kama pinde vinavyounganishwa kwa madaraja. Kisiwa cha kusini kabisa ni "Key West" ambayo kipo kwa umbali wa 140 km pekee na Kuba.
Hakuna milima, na mahali pa juu kabisa pana kimo cha 105 m juu ya
UB
.
Mji mkuu wa jimbo ni
Tallahassee
, na
Jacksonville
ni mji mkubwa jimboni. Miji mingine mikubwa ni
Tampa
,
Orlando
na
Miami
. Orlando kuna maonyesho mashuhuri wa
Disney Land
. Florida ni pia mahali ambako makombora na vyombo vya angani vya Marekani hurushwa kwenye uwanja wa
Cape Canaveral
unaoitwa pia "Kituo cha Angani cha Kennedy".
Florida ni kati ya majimbo ya Marekani yenye wakazi wasio wachache ambao hawatumii
Kiingereza
kama lugha ya nyumbani; takriban 16% husema
Kihispania
.
Kuna wazee wengi kwa sababu ya hali ya hewa pasipo na baridi. Wazee wengi kutoka majimbo ya kaskazini wamependa kuhamia Florida ama kwa uzeeni au kununua makazi wanapokaa wakati wa baridi.
Florida ilikaliwa na Waindio kabla ya kuja kwa Wazungu. Tarehe
2 Aprili
1513
Mhispania wa kwanza alifika Florida na kutangaza utawala wa
Hispania
juu ya rasi. Florida ilitawaliwa kama mkoa chini ya Ufalme Mdogo wa Hispania Mpya.
Baada ya vita ya miaka saba
1763
Hispania ilipaswa kuiachia Uingereza lakini 1783 rasi ilirudi Hispania. 1819 eneo la jimbo liliuzwa kwa Marekani.
3 Machi
1845
Florida ikawa jimbo la 27 la Marekani.
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
|
Makala hii kuhusu maeneo ya
Marekani
bado ni
mbegu
.
Je unajua kitu kuhusu
Florida
kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|