Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Daudi Lekuta Rudisha
(aliyezaliwa
17 Desemba
1988
) ni Mkenya mkimbiaji wa umbali wa kati.Yeye ndiye anashikilia rekodi ya Olimpiki na ya dunia ya mbio za mita 800.
[1]
Alizaliwa mjini Kilgoris, Wilaya ya Trans Mara nchini
Kenya
.Rudisha alienda shule ya St Patrick,shule ya upili ya Kimuron huko Iten, Wilaya ya Keiyo, ambayo inajulikana kwa kuwalea wakimbiaji kadhaa ikiwa ni pamoja na Wilson Kipketer aliyekuwa ameshikilia rekodi ya mbio za mita 800m kwa miaka kadhaa kabla ya Rudisha kujiunga na shule hiyo. Mnamo Aprili 2005 Japheth Kimutai alipendekeza Rudisha kwa James Templeton, na Rudisha akajiunga na kundi la wakimbiaji linalosimamiwa na Templeton.