Aleksander Mikhailovich Prokhorov ( 11 Julai 1916 ? 8 Januari 2002 ) alikuwa mwanafizikia kutoka nchi ya Urusi . Hasa alichunguza mionzi ya aina mbalimbali na kuvumbua leza . Mwaka wa 1964, pamoja na Nikolai Basov na Charles Townes alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia .