Yvette Nipar (amezaliwa 20 Oktoba 1964 ) ni mwigizaji wa filamu na tamthiliya kutoka nchi Marekani . Huenda akawa anafahamika zaidi kwa kucheza kama Agent Kate Jensen katika filamu ya "Walking Tall: The Payback" na "Walking Tall: Lone Justice". Vilevile alicheza Agent Wendy Robbins katika filamu ya "Submerged". Pia anafahamika sana kwa kucheza kama Detective Lisa Madigan katika mfululizo wa kipindi cha televisheni cha "Robo Cop".