Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Wazinza
ni
kabila
la
watu
kutoka eneo la
kusini
-
magharibi
kwa
Ziwa Viktoria
na
visiwa
vya jirani, nchini
Tanzania
.
Lugha
yao ni
Kizinza
.
Mwaka
1987
idadi
ya Wazinza ilikadiriwa kuwa 138,000
[1]
. Wazinza ni kabila dogo lakini lina mambo makubwa liliyoyafanya hapo kale; baadhi ya hayo ni
uhunzi
na
ususi
.
Kazi
yao ilikuwa
uvuvi
,
ufugaji
na
uwindaji
pamoja na
kilimo
. Kwa sasa wamejikita katika anga la wasomi maana wametapakaa kila
taaluma
na kila mahali.
Wazinza walio wengi hupenda kula
ugali
wa
mhogo
,
ndizi
,
samaki
(hasa
sato
,
sangara
,
mumi
,
kamongo
,
dagaa
,
mbete
,
nshonzi
) na
nyama
.
Lakini pia kutokana na uhaba wa
vyakula
hivyo na mgawanyo wa makazi na kazi, Wazinza wamekuwa wakila vyakula vya aina nyingine nyingi. Mfano ni
wali
, ugali wa
mtama
, ugali wa
mahindi
,
mboga za majani
kama vile
msusa
,
kisamvu
,
mchicha
, n.k.
Vyakula asilia kama
maboga
,
viazi vitamu
, mihogo mitamu,
kunde
,
maharage
ni miongoni mwa vyakula muhimu sana kwa Wazinza.
|
Makala hii kuhusu utamaduni wa
Tanzania
bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu
Wazinza
kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|
- ↑
[1]