Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Warshawa
(kwa
Kipoland
:
Warszawa
; kwa
Kiingereza
Warsaw
) ni
mji mkuu
wa
Poland
pia
mji
mkubwa wa nchi, wenye wakazi
milioni
mbili
hivi (1.78 mln - 2018).
Warshawa iko katikati ya
bonde
la
mto Vistula
(Kipoland: polnisch Wisła, takriban
km
350 kutoka
Bahari Baltiki
.
Warshawa imekuwa mji tangu
karne ya 13
, ikawa mji mkuu wa Poland mwaka
1596
.
Iliharibiwa mara nyingi katika
historia
yake, hasa wakati wa
vita kuu ya pili ya dunia
. Wapoland walijaribu kuasi dhidi ya Wajerumani walioshika mji kati ya miaka
1939
na
1944
; pamoja na vifo vingi,
asilimia
90 za
nyumba
zote ziliharibiwa.
Baada ya
vita
mji ulijengwa upya mara nyingi kwa kurudisha nyumba zinazofanana na nyumba za kale.
Kitovu
chake kimeorodheshwa na
UNESCO
kati ya mahali pa
Urithi wa Dunia
.
Kuna
vyuo
66 pamoja na
Chuo Kikuu cha Warshawa
,
vyuo vikuu
vingine, nyumba za maigizo,
opera
na
makumbusho
mbalimbali.
Warshawa ni mji wa
viwanda
vingi vya kutengenezea
chuma
,
mashine
,
motokaa
na mengine mengi.
|
Makala hii kuhusu maeneo ya
Poland
bado ni
mbegu
.
Je unajua kitu kuhusu
Warshawa
kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|