Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Wapogolo
ni
kabila
la
watu
kutoka kusini-kati ya nchi ya
Tanzania
, hususan
mkoa wa Morogoro
.
Lugha
yao ni
Kipogolo
.
Mwaka
1987
idadi
ya Wapogolo ilikadiriwa kuwa 185,000
Inasemekana
asili
yao ni
Afrika Magharibi
, hasa katika nchi ya
Senegal
, pia
Afrika ya Kati
(
Kongo
). Kuna
mila
nyingi Senegal na
ngoma
zake nyingi zinafanana na
Sangula
.
Sababu ya kuhamia Tanzania ilikuwa utafutaji wa
ardhi
ya
kilimo
na mabadiliko ya
hali ya hewa
. Waliendelea kuhama zaidi na wengine walikimbilia pia
Zambia
,
Zimbabwe
na
Malawi
. Ndiyo maana kuna
ukoo
mkubwa wa Matimba kule Malawi na Zimbabwe.
Chakula
kikuu cha Wapogolo ni
wali
na
samaki
na makazi yao ni sehemu za ardhi zenye
rutuba
ambazo hufaa kwa
kilimo
cha
mpunga
na shughuli za
uvuvi
.
Wapogolo wakati wa
masika
huwa na shughuli za utafutaji, hasa shughuli za kilimo na kwa asili ni watu wanaolima kwa
ujamaa
, yaani
kaya
moja huweza kupika
togwa
na kualika kaya nyingine ziweze kusaidia shughuli za kilimo kwa togwa. Wakati wa masika kaya zote huwa na kazi za
uzalishaji
kwa shughuli za kilimo kwa kulima mpunga na wakati wa
kiangazi
sherehe
nyingi huwa zinafanyika katika
jamii
za Wapogolo.
wakati wa sherehe za kabila la Wapogolo
ngoma
aina ya sangula hupigwa na hii ndiyo ngoma ya asili ya kabila wa Wapogolo. Ngoma hiyo ya sangula hupigwa wakati wa
furaha
kama vile kwenye shughuli za sherehe za
mavuno
, sherehe za kusimikwa
kiongozi
wa ukoo,
matambiko
na n.k.
Katika kaya za Kipogolo wakati wa
jioni
wazee
hupenda kukaa na
wajukuu
kwa lengo la kuwasimulia mambo ya kale yenye mafunzo ili kuwajenga
watoto
hao wanapokuwa wakubwa kujua nini wanapaswa kufanya. Wakati wa mazungumzo hayo huwa wanatafuta pepeta. Pepeta ni
kitafunwa
kinachotokana na
zao
la mpunga, huandaliwa kwa kuchukua mpunga mteke (mpunga usiokomaa) na kuukaanga, kisha kuutwanga na kutengeneza pepeta. Ni moja kati ya kitafunwa cha kiburudisho kwa kabila la Wapogolo.
|
Makala hii kuhusu utamaduni wa
Tanzania
bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu
Wapogolo
kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|