Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Historia
(kutoka Kigiriki
ιστορια
, historia; pia "tarehe" kutoka
Kiarabu
?????
tarih
kwa maana ya "historia": pia tena "mapisi") ni somo kuhusu
maisha
ya
binadamu
na
utamaduni
wao
wakati
uliopita.
Mara nyingi neno hilo lina pia maana ya maarifa yoyote kuhusu wakati uliopita, yawe au yasiwe maarifa ya watu (kwa mfano "historia ya ulimwengu").
Historia ni hasa mfululizo wa habari za mambo yaliyotokea pamoja na sababu zake.
Binadamu anaziandika ili kuelewa maisha yake, yaani ametokea wapi, amepata mafanikio gani na matatizo gani.
Historia inatufundisha kuishi: kumbukumbu za mambo ya zamani (
vita
,
uhuru
, viongozi na mengineyo) zinatuwezesha kuendelea vizuri zaidi.
Wanahistoria wanapata maarifa yao kutoka
maandishi
ya zamani (hasa kwa
historia andishi
), kutoka
fasihi simulizi
na kutoka
akiolojia
(hasa kwa
historia ya awali
).
|
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu
Historia
kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|